Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kunyakua tuzo ya Woman of the future waliyoshinda kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kampuni hiyo ilishinda kwa kuajiri zaidi ya asilimia 40 ya wanawake kwenye menejimenti yake. Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd waliandaa tuzo za Rising Woman zenye lengo la kuwezesha wanawake kuvunja upendeleo kwenye ajira nchini.
Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa (kulia), Mkurugenzi wa Rasilimali watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis (katikati ) na Meneja wa Mawasiliano Vodacom Tanzania Plc, Alex Bitekeye wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya Woman of the future waliyonyakua kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kampuni ya Vodacom ilishinda kwa kuwa na zaidi ya asilimia 40 ya wanawake katika menejimenti. Tuzo hizo za The Citizen Rising Woman ziliandaliwa na kampuni ya Mwananchi communications Ltd.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...