Na Muhidin Amri,Tunduru

WAKULIMA wa korosho wilayani Tunduru,wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kutoa viuatilifu na mbegu za korosho kwa wakulima bure katika msimu wa kilimo 2021/2022,jambo lililo hamasisha wakulima wengi kufufua mashamba yaliyotelekezwa kwa muda mrefu na kuongeza ukubwa wa mashamba yao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana mjini Tunduru walisema, hatua hiyo ya Serikali imesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji wa korosho kutoka kilo milioni 24, msimu 2020/2021 hadi kufikia kilo milioni 25,284,493 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya kilo laki 2.

Said Malembe alisema, uzalishaji wa korosho katika msimu 2021/2022 ulikuwa mzuri ikilinganisha na msimu uliopita na sababu kubwa ni upatikanaji wa viuatilifu bora na vilivyotolewa kwa wakati na Serikali.

Malembe alisema, hata utaratibu wa malipo ya fedha kwa wakulima waliouza korosho zao kupitia minada mbalimbali ulikuwa nzuri, kwani walipata fedha baada ya wiki moja au mbili tangu walipouza korosho zao tofauti na miaka ya nyuma ambapo utaratibu wa malipo haukuwa mzuri.

Ali Mfaume,amekipongeza Chama Kikuu cha Ushirika(TAMCU LTD)kupitia vyama vya msingi vya ushirika(Amcos)kusimamia vizuri ugawaji wa viuatilifu hivyo kwa wakulima pamoja na kusimamia minada ya korosho iliyofanyika katika maeneo mbalimbali.

Alisema, iwapo serikali itaendelea na utaratibu wa msimu uliopita kutoa pembejeo bure na malipo kufanyika kwa wakati, basi wakulima wengi wataendelea kulima na hivyo kuongezeka kwa uzalishaji wa zao hilo katika mkoa wa Ruvuma.

Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika wilayani humo Imani Kalembo, amewapongeza wakulima wanahudumiwa na Chama hicho kwa kuvuka malengo ya uzalishaji wa zao korosho katika msimu wa kilimo 2021/2022.

Kwa mujibu wa Kalembo katika msimu huo, malengo ilikuwa kuzalisha kilo milioni 25 tu,lakini wamefanikiwa kuzalisha ziada ya kilo 284,493 na kufanya jumla ya korosho zilizozalishwa kufikia kilo milioni 25,284,493 ikilinganisha na msimu uliopita ambapo wakulima walizalisha kilo milioni 15.

Alisema,korosho hizo zilikusanywa katika vyama vya msingi na kuuzwa kupitia minada 13 ambapo wastani wa bei ilikuwa Sh. 2,802 kwa kilo moja na kufanya fedha zilizoingia kwenye mzunguko kutokana na zao hilo kufikia Sh.bilioni 50.534,028,825.

Kalembo alisema, kati ya fedha hizo wakulima wamepata Sh.bilioni 44,549,443,214.83 na Sh.bilioni 5.984,686,648.87 ni tozo za kisheria kwa ajili ya kulipia magunia,ushuru wa Halmashauri na gharama za usafirishaji.

Aidha alisema, katika msimu wa mwaka jana wakulima wengi wamepata fedha zao na hata wale ambao bado hawajalipwa kutokana changamoto mbalimbali,wanaendelea kuchukua hatua ili kuhakikisha wakulima hao wanalipwa fedha zao.

Alisema, uzalishaji huo umechangiwa sana na matumizi sahihi ya pembejeo na viuatiifu bora vilivyotolewa bure na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan,ambaye tangu alipoingia madaraka ametoa ushirikiano mkubwa kwa wakulima wa korosho.

Pia alisema, kutokana na hamasa kubwa ya wakulima katika msimu uliopita ni mategemeo yao kwamba uzalishaji wa korosho katika msimu 2022/2023 utaongeza kutoka tani elfu 25 hadi kufikia tani elfu 32 na kuwataka wakulima kuanza kupalilia mikorosho yao mapema.

Aliongeza kuwa, katika msimu huu pembejeo zitaletwa mapema ambapo wakulima watachangia asilimia 50 na Serikali itachangia asilimia 50 kama sehemu ya mkakati wa kuendeleza zao hilo ili kuongeza uzalishaji.

Mwenyekiti TAMCU)Mussa Manjaule alisema,chama hicho kimeweza kulipa wakulima wote aliopeleka korosho zao kwenye minada na hakuna mkulima ambaye anadai fedha zake.

Alisema, wamefanikiwa kufika malengo ya uzalishaji kutokana na kujipanga vizuri na kuwa na ushirikiano mkubwa kati ya viongozi wa chama,maafisa ugani na viongozi wa ngazi mbalimbali ambao kwa pamoja walifanya kazi nzuri ya kutoa elimu juu ya kilimo bora cha korosho na kuhamasisha matumizi bora ya viuatilifu.
MWISHO.
,493 kati ya lengo la kuzalisha kilo milioni 25 na kuwa Chama cha kwanza kulipa madeni yote ya Wakulima.

Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Imani Kalembo akizungumzia hali ya uzalishaji wa zao la Korosho katika msimu wa kilimo 2021/2022 ambapo wakulima wanaohudumiwa na Chama hicho walifanikiwa kuzalisha kilo milioni 25,284,,493

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...