Adeladius Makwega-DODOMA

Katika Makala iliyotangulia tulitazama baadhi ya koo za Kimaasai namna zilivyokuwa na utani ndani yake na pia nilitazama maana na asili ya majina ya baadhi ya koo chache nilizokutajia.

Kwa siku ya leo naendelea kulitupia jicho kabila hili la Wamaasai, ndani ya kabila hili kuna mgawanyo kazi huwa katika rika.

Kwanza kabisa LAYON (ILAYON) hawa ni rika ya vijana wadogo wa kiume ambao kazi yao kubwa ni kuwasaidia morani kuchunga mifugo au wakati mwingine kutafuta kuni za kupikia. Pia wakifahamika kama LIKINDOONYO (VORUO) hawa ni ikimaanisha ni wale wanaobeba na kuleta chakula kwa wakubwa.

Rika la pili ni IlMORAN hawa ni vijana wakiume ambao tayari wameshapitia jandoni, kazi yao kubwa ilikuwa ni kulinda jamii yao, kuteka mifugo na kwenda vitani kupigana..
Hawa jamaa wana utani unaofahamika kama ENGANG au boma, utani huu huwa kwa morani walioa nyumba moja au wale waliokwenda tohara pamoja.

Hapa kuna kundi ambalo ni la watu wazima, hawa jamaa wana utani wa rika lao tu kwa kusema wewe kijana vipi? Wakati huyo anayeambiwa huwa si kijana yaani si NGANYONI.


Hapa msomaji wangu unapaswa kufahamu kuwa hawa morani huwa ni ILKIK, LIKIVONI, LINDLOLIK. Hawa watu wazima huwa LIMESKUK, LINWATI, LINDERITO na LINDILALA.

Hapa inaaminika kuwa LAIBON wote huwa LINDILALA. Kwa desturi LAYONI hawezi kutaniana na LAIBON.

Nao wanawake wa Kimaasai hugawanywa katika makundi makubwa matatu , la kwanza wale waliofanyiwa tohara pamoja, wale walioolewa na wale akinana wazee.

Wanawake waliolewa wanaweza kuwataniana na vijana wa kiume wadogo kama MORUAI hasa hapa kama anahitaji kumuagiza kitu au kupata kitu kutoka kwake.

Wakati Moran anaweza kumtania binti kigori kwa kumwambia ESANJA

ESANJA akimaanisha MCHUMBA WANGU

ENGITOK akimaanisha MWANAMKE.

Utani huu huwa mbaya kwani unaweza ukazaa matunda ya utani alafu kusababisha watu kuachana na kufanya wengine hadi kuwa wapenzi na kuleta migogoro kwenye ndoa au mwanamke huyo anayetaniwa kuolewa na yule mtaniaji.

Wamasai wamekuwa na desturi ya kuapa pale anaposema jambo la hatari na kiapo chao huwa kwa jina la baba yake au mumewe.

NYANGUSU LAINEI MAYOU akimaanisha kuwa NYANGUSI JAMBO HILI SILITAKI.

Mwanamke Kimasai uapa kwa kusema.


APAA NYANGUSU LINDWATI

Hii nayo ikiwa namaana kama ya kiapo cha mwanamke huyo kwa mwanaume.

Pia katika Lugha ya Kimasai neno SINDA AI maana yake mume au mke asiye halali

Basi mwanakwetu kwa leo naishia hapo. Kipi kitaeendelea subiri matini ijayo.

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...