Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
MHIFADHI Misitu Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro Robert Mwangosi ameelezea jinsi wilaya hiyo ilivyojipanga kipindi hiki kwa ajili ya kupanda miti itakayowesesha kuweka hali nzuri ya Mazingira pamoja kusaidia kupatikana kwa hewa safi inayotegemewa na kila mmoja wetu.
Akizungumza wakati wa tukio la upandaji miti katika Wilaya hiyo,Mwangosi amesema wao kama wakazi wa wilaya ya Gairo kutoka TFS kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Gairo wamejipanga vyema na wamekuja na kauli mbiu na mikakati madhubuti katika kukabiliana na hali ya jangwa na mikakati ya Gairo yenye urithi wa kijani.
"Tumefanya mipango mbalimbali ya kujidhatiti ya upandaji miti ikiwa ni kuanzisha clubs, kuweka mbinu mbalimbali, kuwaunganisha wanafunzi kwa pamoja kuweza kupanda miti na kuweka miundo mbinu ya kufanya wanafunzi waweze kupenda mazingira na tumefanikisha kila mwanafunzi ana mti mmoja anaoweza kuusimamia toka ameingia shule hadi atakapo maliza," amesema Mwangosi
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabiri Makame amesema kampeni ya urithi wa kijani Gairo, ni kampeni inayolenga kuibadilisha wilaya hiyo na kuwa ya kijani kwa kufanya harakati za upandaji wa miti na kuweza kutoa elimu kwa jamii juu ya suala zima la uhifadhi wa mazingira ili wilaya hiyo itoe mchango mkubwa katika kumuunga mkono Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika harakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya Nchi.
Wananchi wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wakielekea kwenye moja ya maeneo kwa ajili ya kupanda miti ikiwa ni sehemu ya Wilaya hiyo kutunza mazingira kwa kupanda miti
Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wakishiriki tukio la upandaji miti ikiwa ni mkakati wa Wilaya hiyo kuendelea kutunza Mazingira pamoja na uhifadhi.Miti hiyo inepandwa kutokana na ishi kati ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Gairo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...