Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk.Damas Ndumbaro ametia saini mkataba wa uenyeji (Host Agreement), kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Utalii kwa Kamisheni ya Afrika (65th United Nations World Tourism Organization Regional Commission for Africa), utakaofanyika tarehe 5 hadi 7 Oktoba 2022, mjini Arusha.

Sherehe za utiaji saini zimefanyika Machi 7 mwaka huu katika makao makuu ya Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) na kuhudhuriwa pia na Ubalozi unaowakilisha wa Ufaransa unaowakilisha pia Uhispania na UNWTO.

Kabla ya utiaji saini, ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Ndumbaro pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Uhispania Samwel W. Shelukindo kilifanyika kikao na kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano.

Dkt Damas Ndumbaro (Mb), Waziri wa Maliasili na Utalii akitiliana saini mkataba wa uenyeji (Host Agreement) na Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO),katika makao makuu ya Shirika hilo mjini Madrid, Uhispania.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Mhe. Damas Ndumbaro (Mb), Waziri wa Maliasili na Utalii ukiwa katika mkutano kabla ya utiaji saini wa mkataba wa uenyeji na ujumbe wa UNWTO ulioongozwa na Bw. Zurab Pololikashvili, Katibu Mtendaji wa UNWTO. Wengine katika picha kwa upande wa Tanzania, ni Mhe. Balozi Samwel W.Shelukindo, Balozi wa Tanzania na Bw. Amos Tengu, Afisa Ubalozi

Dk.Damas Ndumbaro ambaye ni Waziri wa Maliasili na Utalii akibadilishana hati za makubaliano ya uenyeji wa mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Utalii kwa kanda ya Afrika na Bw. Zurab Pololikashvili, Katibu Mtendaji wa UNWTO kwa ajili ya kuangalia maeneo ya ushirikiano


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...