Na. Dennis Gondwe, DODOMA

WANAWAKE katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kukamilisha malipo ya umiliki wa viwanja wanavyomiliki kwa mujibu wa sheria ili kuonesha uwajibikaji katika jamii.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkaguzi wa Ndani katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, CPA Jestina Naftal katika mahojiano maalum kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika Halmashauri ya Jiji la Dodoma mwishoni mwa wiki.

CPA Naftal alisema kuwa wanawane ni wawajibikaji wazuri sana katika mambo ya maendeleo. “Nafahamu wapo wanawake wanaomiliki viwanja katika halmashauri ya Jiji la Dodoma lakini hawajakamilisha malipo ya umiliki wa viwanja hivyo. Nashauri na wenyewe waweze kukamilisha malipo hayo. Wanawake tuwe mstari wa mbele sababu tunaposimama kuzungumzia jambo fulani huwa linasikika sana na kueleweka kwa jamii nzima. Hivyo, tutumie ushawishi wetu kuwahimiza wanawake wenzetu kukamilisha malipo hayo ili kujihakikishia umiliki wa viwanja kwa mujibu wa sheria” alisema CPA Naftal.

Akiongelea fursa zilizopo kwa wanawake katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, alizitaja kuwa ni mikopo isiyo na riba inayotolewa kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. “Tunaona wanawake wengi wameanza kunufaika na mikopo hiyo, hivyo, ni fursa kwao. Tumeona vikundi vingi vimenufaika katika kilimo, mifugo na ujasiliamali. Tuna mifano ya wanawake waliokopa na kurudisha na kupata maendeleo mazuri. Wengine kwa ajili ya shughuli za kilimo na viwanda vidogovidogo” alisema CPA Naftal.

Fursa nyingine ni kunufaika na ushauri wa kitaalam kutoka halmshauri ya Jiji la Dodoma. “Bahati nzuri jiji lina wataalam ngazi ya kata. Wanawake pia wanapohitaji ushauri wa kitaalam huwa ni rahisi kuupata kupitia maafisa ugani hao” alisisitia CPA Naftal.

Mkaguzi huyo wa ndani aliwashauri wanawake kuzitafuta fursa za maedeleo kwa bidii. “Kupitia maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, ushauri wangu kwa wanwake wa Jiji la Dodoma, nawashauri wajitokeze kutafuta fursa za kujiletea maendeleo. Jiji linazo fursa nyingi, wanawake wajitokeze kunufaika na fursa hizo” alisisitiza CPA Naftal.

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka 2022 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Kizazi cha haki na usawa kwa naendeleo endelevu, tujitokeze kuhesabiwa” na ngazi ya Mkoa wa Dodoma yatafanyika wilayani Chemba.

Mkaguzi wa Ndani Halmashauri ya Jiji la Dodoma, CPA Jestina Naftal

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...