WATANZANIA wametakiwa kuzingatia afya ya kinywa na meno kwa kuwa ndio ufunguo wa kuwa na siha njema.

Kauli hiyo imetolewa na mtaalamu wa masuala ya afya ya kinywa na meno, Dk Donna Williams- Ngirwa (pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Afya ya Kinywa na Meno.

Alisema ipo haja ya watanzania kuhakikisha kwamba wanashughulika na afya ya kinywa na meno kwa kuwa ndio mlango wa uhai na afya bora katika maisha yao.

 Alisema katika mahojiano leo kuwa mtu akizimbea kushughulikia afya ya kinywa anakaribisha maradhi mbalimbali yakiwemo yaliyo sugu.

Dk Donna  wa Afya Bora Complete Dentistry  Ltd alisema kwamba maadhimisho ya mwaka huu yenye kauli mbiu ya kimataifa ya ‘jivunia kinywa chako’ yana maana kubwa  kwa kuwa kuzuia maradhi ya kinywa kwa kumtembelea daktari wa meno angalau mara mbili kwa mwaka husaidia sana.

 “Magonjwa mengi ya kinywa na meno hayajitambulishi mpaka yamefikia hatua mbaya hivyo ni vyema kuwahi kuyagundua, ili uwe na siha njema”  alisema.

 Hata hivyo alitaja kuwepo na kampeni kubwa ya  afya ya kinywa ili kujiweka sawa kama ufanyaji wa mazoezi unavyotumika kuweka sawa mwili.

 “Kuna haja ya kuanzisha kampeni ya kuelimisha umma umuhimu wa afya ya kinywa kwa kuwa ndio mlango wa afya,”  alisema na kuongeza kwamba ni watu  waone umuhimu  wa kujua wanachokula na madhara yake kwani ndio msingi wa afya njema ya meno na kinywa.

 Anasema watu hawafikirii kuhusu uhusiano uliopo kati ya afya ya kinywa na afya yao kwa ujumla, kwani kinywa ndio ukuta wa kuzuia maradhi katika mwili.

Anasema maradhi ya kinywa yanapokuwa katika hatua za mwanzo ni rahisi kutibika lakini yanapokuwa katika hatua kubwa yanakuwa changamoto.

"Mtu anapokuwa na tatizo la kinywani huongeza hatari , kwa mfano ugonjwa wa rheumatoid arologist, atherosulinosis, shinikizo la damu, ugonjwa wa Alzheimers, ugonjwa wa sukari, na matatizo wakati wa kujifungua."

Alisema watu wanaougua matatizo ya kinywani , huwa na sababu tofauti zinazoweza kusababisha magonjwa mengine.

Kwa mfano, idadi kuu ya molekuli zinazozalishwa na seli za binadamu na kusababisha uvimbe katika ufizi zinaweza kufikia viungo vingine vya mwili na kusababisha athari katika maeneo hayo. Kumtembelea daktari wa meno ili kutibu matatizo hayo ya kinywa ni muhimu.

Dk Donna   amesema kwa sasa wataalamu wa afya ya kinywa wamekuwa na vifaa vya kisasa zaidi hivyo ni rahisi kubaini matatizo kabla hayajawa sugu.

“Kwa mfano ninapofanya shughuli zangu tunafuata misingi ya kimataifa ya utoaji huduma kutokana na umuhimu wake,” alisema na kuongeza kuwa sekta hiyo ina teknolojia mpya.

Dk Donna  ambaye pia alishiriki kuanzisha  kliniki ya afya ya kinywa ya  Morningside Dental Care, ya New York, Marekani mwaka 1995, alisema njia nzuri ya kuwezesha afya ya kinywa na meno ni kuhakikisha kwamba unamuona daktari wa meno ili aweze kukusaidia.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...