Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa  Taasisi ya Sekta Binafs  TPSF  Bi.Angelina Ngalula akisalimiana na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dk,Mehment v Gulluoglu 

Wafanyabiashara  wa Ndani ya nchi wametakiwa kuendelea kukuza  ushirikiano na Wafanyabiashara wengine kutoka nje ya nchi   ikiwemo wafanyabiashara kutoka n nchi ya Uturuki ili kuhakikisha Wanakuza na  kuongeza thamani ya Mnyoro wa Uchumi wa nchi.

Wito huo Umetolewa na Ndugu.Paul koyi Rais wa chemba ya Biashara  Viwanda na kilimo(TCCIA) Wakati wa Mkutano wa siku moja wa Wafanyabiashara na wekezezaji zaidi 25 kutoka nchini Uturuki na wandani ya nchi ikiwa lengo Kubadilishana uzoefu na kupeana Fursa za Uwekezaji pande hizo mbili.

Ndugu Koyi Amesema kuwa lengo la serikali nikuhakisha Wana wapa Fursa Wafanyabiashara na wawekezaji wa Ndani ya nchi kutafuta masoko na kuwekeza nje ya nje ikiwa lengo kukuza Ushirikiano katika Uwekezaji.

Hata hivyo  amesema kuwa Miongoni mwa mwa  vitu wanavyo peleka nchini Uturuki ni Malighafi ya mazao hivyo basi wanaomba Wafanyabiashara kupeleka  nchini humo  kwa wingi na kuongeza ongezekao la thamani ikiwa lengo ni kuchochea Uchumi wa nchi na wakulima kwa Ujumla ili wanufaike na kilimo.

Wakati huo huo Amesema kuwa Miongoni mwa makampuni yalio kuja nchini kushiriki  kutoka nchini Uturuki ni ya Umeme hivyo wamekutana na Wafanyabiashara Biashara wa Ndani wanaofanya Biashara ya vifaa vya Umeme hapa Tanzania ili wapeane Fursa za Uwekezaji.

Naye Mwenyekiti wa  Taasisi ya Sekta Binafs  TPSF  Bi.Angelina Ngalula amesema kuwa  Biashara ya nchi ya Utuluki na Serikali ya Tanzania imeendelea kukua na kufikia kipindi Cha Mwaka Mmoja  Dora  Milioni Mia Tatu tofauti na Zamani ilikuwa Dora Milioni Miambili na Hamsini Ndani ya Kipindi Cha Mwaka Mmoja imekua zaidi  hivyo Kupitia juhudi Rais  Jamhuli ya Muungano Wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassani .

Aidha Bi. Ngalula  amesema kuwa Utuluki Ina mpango wa kujenga Vituo vyao hapa Tanzania vya  kuweza kuonesha Fursa ambazo zinapatoka nchini Uturuki kwa kushirikiana na Watanzania ili kuhakikisha wanachochoea Uchumi wa nchi hasa katika kuwainua Watanzania. 

Mkutano huo ulifanyika Jijini Dar es salaam na Kushiri Wafanyabiashara na Wawekezaji Tofauti katoka Ndani nchi na nchi ya Utuluki ulio andaliwa na nchi Uturuki Chini ya Balozi wa nchi hiyo 

Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dk,Mehment v Gulluoglu kwa Kushirikiana na Serikali ya Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...