Na.Vero Ignatus,Arusha


Wazazi/Walezi wametakiwa kuacha tabia ya kuwabagua watoto Jambo ambalo limekuwa likileta chuki,matabaka na hupelekea kusababisha Ukatili Kati yao.


Hayo yamesemwa na Mwinjilisti Benson Materu katika ibada ya jumapili katika kanisa la KKKT Usharika wa Engarenarok,Dayosisi ya Kaskazini Kati kuwa Wazazi wengi wamekuwa wakiwathamini watoto wenye uwezo na kuwaona wasiokua nacho hawana thamani na kusababisha uchonganishi

"Mungu amewapa watoto hao wote ni wa kwako,wawe na mafanikio ama la! hata Kama unao watoto kumi jitahidi kuchukuliana nao, wametofautiana,wengine wanao uwezo mkub wa wengine hawana kabisa,wapende hivyohivyo usiwabague watie moyo waombee ili wafikie malengo yao.alisema Materu

Materu aliwataka waumini hao kutokukaa kimya pale wanapoona Ukatili unapotendeka kwani husababisha maumivu kwa watendelewa wa tendo hilo na kuweka majeraha na makovu yadiyotibika kwa haraka.

Asilimia kubwa ya Ukatili wanaofanyiwa watoto huwa unaanza ngazi ya familia wakiwemo ndugu wa karibu wa baba au mama,huku wakati mwingine wamekuwa wakiwatishia watoto kutokusema juu ya vitendo wanavyowafanyia.

Aliendelea alifafanua kuwa ukatili ni kitendo anachotendewa mtu yeyote kwa makusudi ili hali anafahamu fika kitaleta madhara kwa muhusika au maumivu yasiyotibika kwa haraka

"Ifahamike kuwa maana halisinya Ukatili kitendo chochote Cha UKATILI anachofanyiwa mtu kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza kisaikolojia,kimwili,kingono au kiuchumi kwa sababu ya jinsia yake,kwa makusudi"alisema

Akizungumza mmoja wa waumini kutoka kanisani hapo bi Oliva Wenceslaus amesema kuwa kwenye jamii anayotokea wazazi wana tabia hiyo ya kubagua watoto kwani mtoto wa kwanza ni wa baba wa pili ni wa mama watatu anakuwa wa upande wa baba,hivyo inaleta sana mkanganyiko kwenye jamii haswa kwa watoto wenyewe

Amesema kuwa asilimia kubwa kutokana na hulka hiyo, wasichana wakiolewa wanatumia ubini wa mama, badala ya kutumia wa baba kwani misingi hiyo imetokana na kubaguliwa tangia wakiwa watoto wadogo

Amesema kuwa akubwa kwenye jamii yetu wanaochangia uaguzi huo ni babu na bibi kwa kuwaita watoto kuwa ni wajina la bibi mzaa mama au babu, mzaa baba,na mwingine jina la babu mzaa mama,wazazi wengine wanawatenga watoto hata kuwalipia ada inakuwa mtihani mkubwa.

Aidha Kwa mijibu wa Umoja wa Mataifa (UN)UKATILI huu umetafsiriwa Kama kitenda anachofanyiwa mtu yeyote awe mwanamke ,mwanaume au mtoto ambacho kimelenga kumuumiza mwili au kiutu.

Sambamba na hayo pia upo Ukatili wa aina mbalimbali ikiwemo wa UKATILI wa Kimwili, kisaikolojia,Ukatili wa Kiafya,Kingono na Ukatili wa kiuchumi

Madhara yanayoweza kumpata mtu aliyetendewa Ukatili,ni mpamoja na kukosa ujasiri,hukitenga,hawezi kumwamini mtu mwingine,humpelekea kupata msongo wa mawazo,anaweza pia kumpelekea kupoteza maaisha .

Hivyo Jamii haipaswi kukaa kimya pale wanapoona viashiria vyovyote vya Ukatili vikitendeka ni vyema kutoa taarifa mapema ili kuzuia visiendelee .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...