Na Damian Kunambi, Njombe.

Kufuati kusambaa kwa taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa mlipuko wa Polio nchini Malawi, baadhi ya Wilaya hapa nchini zilizopo mipakana mwa nchi hiyo ikiwemo Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe zimeanza kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo kwa kuanza kampeni shirikishi ya chanjo ya Polio.

Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi wilayani Ludewa Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Stanley Mlayi amesema tayari wameshaandaa timu ya kuendesha zoezi hilo la utoaji chanjo ambalo litafanyika kuanza tarehe 24 mpaka 27 mwezi huu na litahusisha watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano.

Amesema tayari wameshaunda timu ya kuendesha zoezi hilo ambalo litafanyika katika vituo vya afya pamoja na kuzunguka nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata chanjo na watakaochanjwa watakuwa na alama itakayowaonyesha kuwa tayari wamepatiwa chanjo hiyo.

Sanjari na hilo mganga mkuu amesema kuwa kumekuwa na upotoshaji kwa baadhi ya watu juu ya chanjo mbalimbali zitolewazo kitu ambacho kinawapa mazingira magumu ya kufanikiwa hivyo ameiomba kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kufanya upotoshaji huo.

"Kwa sasa zoezi la kutoa chanjo yoyote ile limekuwa gumu katika jamii, wakati timu husika inapita kutoa elimu ya watu kupata chanjo huku nyuma watu wengine wanapita kuwapotosha watu kutopata chanjo, yaani watu wamekuwa wepesi kuelewa kampeni za kisiasa kuliko kampeni za chanjo", Amesema Mlayi.

Aidha kwa upande wake Mratibu wa chanjo wilayani hapo James Kadege amesema kuwa chanjo hiyo itawahusu watoto wote walio na umri chini ya miaka mitano na hata kama alikwisha pata atalazimika kupatiwa tena ili kujiridhisha na chanjo mpya kwani inawezekana awali alipatiwa lakini haikuwa imekamilika.

Ameongeza kuwa utoaji wa chanjo hii wakazi wa mwambao watapewa kipaumbe zaidi kwakuwa ukanda huo ndio upo jirani zaidi na nchi ya Malawi hivyo amewaomba wananchi wote wa mwambao na Ludewa kwa ujumla kuhakikisha walengwa wanapata chanjo hiyo.

Linus Malamba ni Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya hiyo ambaye amehudhuria kikao hicho kwa niaba ya mkuu wa wilaya amesema timu hiyo iliyoundwa inapaswa kutoa elimu ya kutosha katika maeneo ya mikusanyiko kama Makanisani, Msikitini na sokoni ili watu waweze kupata uelewa juu ya umuhimu wa chanjo hiyo.

"Watu walikuwa wanapotoshana sana juu ya chanjo ya UVICO-19 lakini pamoja na upotoshaji huo elimu ilitolewa na jambo hili likafanikiwa hivyo ni matumaini yetu pia katika hili elimu ikitolewa litafanikiwa kama yalivyofanikiwa mengine", Amesema Malamba.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Stanley Mlayi akizungumza katika kikao cha Kamati ua Afya ya Msingi ya Wilaya , kwaajili ya uhamasishaji juu ya chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa Linus Malamba akiwa amemuwakisha Mkuu wa Wilaya katika kikao cha kamati ya Afya ya Msingi ya Wilaya Kwa ajilinya uhamasishaji wa chanjo ya Polio.

Mratibu wa Chanjo wilaya ya Ludewa James Kadege akiwasilisha mada katika kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Wilaya, kwaajili ya Uhamasishaji wa chanjo ya Polio.

Baadhi ya Wanakamati ya Afya ya Msingi Wilaya ya Ludewa wakifuatilia mjadala wa namna ya utoaji chanjo ya Polio kwa watoto walio chini ya miaka 5
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...