Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na Balozi wa Tanzania nchini
Uholanzi, Mhe.Irene Kasyanju wakipewa maelezo Meneja Masoko wa Kilabu
ya Ajax Bw. Ted Robinson mara baada ya kutembelea uwanja wa Kilabu
hiyo kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kutangaza vivutio vya utalii
vya Tanzania kupitia jezi na na mbao za matanagazo zilizopo katika
uwanja wa Kilabu hiyo
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na Balozi wa Tanzania nchini
Uholanzi, Mhe.Irene Kasyanju ( kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na
Watumishi wengine wa Ubalozi waliongozana nao kutembelea uwanja wa
Kilabu hiyo mara baada ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Kilabu ya
Ajax kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia
jezi na na mbao za matangazo zilizopo katika uwanja wa Kilabu hiyo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas
Ndumbaro akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe.Irene
Kasyanju wakizungumza na Meneja Masoko wa Kilabu ya Ajax , Ted Robinson
mara baada ya kutembelea duka la jezi za Kilabu ya Ajax
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na Balozi wa Tanzania nchini
Uholanzi, Mhe.Irene Kasyanju wakiwa wameongoza na Meneja Masoko, Ted
Robinson mara baada ya kutembelea uwanja wa Kilabu hiyo kwa ajili ya
kufanya mazungumzo ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania
kupitia jezi na na mbao za matanagazo zilizopo katika uwanja wa Kilabu
hiyo
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania
nchini Uholanzi, Mhe.Irene Kasyanju ( wa pili kushoto) wakiwa pamoj na
Watumishi wa UBalozi wa Tanzania nchini Uholanzi mara baada ya
kutembelea uwanja wa Kilabu hiyo kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya
kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia jezi na na mbao za
matanagazo zilizopo katika uwanja wa Kilabu hiyo
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na Balozi wa Tanzania nchini
Uholanzi, Mhe.Irene Kasyanju akikabidhi zawadi mbali mbali kwa
Bi.Tanja Dik, Afisa Mkuu wa Uwanja wa Ajax na Bw. Han Mouton, Mkurugenzi
wa Fedha wa Kilabu ya Ajax mara baada ya kufanya mazungumzo na
viongozi wa Kilabu hiyo kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii vya
Tanzania kupitia jezi na na mbao za matanagazo zilizopo katika uwanja
wa Kilabu hiyo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas
Ndumbaro akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe.Irene
Kasyanju wakiwa kwenye picha ya pamoja na Afisa Mkuu wa Uwanja wa Ajax
Bi.Tanja Dik, ( wa kwanza kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Fedha wa
Kilabu ya Ajax Bw. Han Mouton ( wa kwanza kushoto) mara baada ya
kufanya mazungumzo na viongozi wa Kilabu hiyo kwa ajili ya kutangaza
vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia jezi na na mbao za matanagazo
zilizopo katika uwanja wa Kilabu hiyo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas
Ndumbaro akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe.Irene
Kasyanju wakiwa kwenye picha ya pamoja na Afisa Mkuu wa Uwanja wa Ajax
Bi.Tanja Dik, ( wa kwanza kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Fedha wa
Kilabu ya Ajax Bw. Han Mouton ( wa kwanza kushoto) mara baada ya
kufanya mazungumzo na viongozi wa Kilabu hiyo kwa ajili ya kutangaza
vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia jezi na na mbao za matanagazo
zilizopo katika uwanja wa Kilabu hiyo, Katikati ni Meneja Masoko, Ted
Robinson wa Uwanja huo
……………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Uholanzi.
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amefanya mazungumzo na Uongozi wa Klabu
ya Soka ya Ajax ya Uholanzi ili itangaze vivutio vya Utalii vya
Tanzania kupitia matangazo ya jezi na mbao za matangazo (billboards)
uwanjani.
Dkt. Ndumbaro
amebainisha hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa
klabu hiyo wakiongozwa na Bi.Tanja Dik, Afisa Mkuu wa Uwanja na Bw. Han
Mouton, Mkurugenzi wa Fedha wa timu hiyo.
Katika mazungumzo
yao, Dkt. Ndumbaro amewasilisha nia ya Tanzania kushirikiana na Klabu
ya Ajax katika kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania kupitia
matangazo kwenye jezi na mbao za matangazo zilizopo katika iwanja wa
klabu hiyo.
“Mazungumzo yetu
yameenda vizuri na viongozi hao wamepokea pendekezo na ombi letu na
kuahidi kulifikisha kwenye idara husika ya biashara pia kuendeleza
mawasiliano na Ubalozi wetu uliopo hapa kuangalia namna ya kutekeleza
nia hii,” amesema Dkt. Ndumbaro.
Katika hatua
nyingine, Mhe. Dk Ndumbaro ametembelea na kufanya mazungumzo na Uongozi
wa Klabu kubwa ya Golf nchini Uholanzi ya GC BurgGolf Westerpark,
Zoetermeer.
Katika mazungumzo
yake na Meneja mauzo na matukio, Bi. Eline Dujardin na Mkufunzi katika
klabu hiyo Bw. Ronald Mos, Dk Ndumbaro amewasilisha pendekezo la
Tanzania kushirikiana na klabu hiyo katika kuandaa tamasha la golf
litakalofahamika kwa jina la “Mt. Kilimanjaro Open”.
Hata hivyo, pendekezo
limepokelewa vizuri na viongozi wa klabu hiyo na kuahidi kuwasiliana
zaidi kupitia Ubalozi ili kuangalia namna bora ya kulitekeleza.
Waziri Ndumbaro
amefanya ziara hiyo ya kikazi nchini Uholanzi kwa lengo la kutafuta
fursa za kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania nchi humo.
Aidha, Waziri Dk
Ndumbaro amepata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Irene F. M.
Kasyanju, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi
pamoja na watumishi wa ubalozi huo.
Akizungumza na
watumishi hao, Dk Ndumbaro amewaeleza mwelekeo wa Wizara katika
kutangaza utalii ikiwemo uanzishwaji wa vifurushi vya wanafunzi
(student package), matumizi ya utangazaji utalii kidijitali ,
Utangazaji kupitia michezo, vyombo vya habari , Watu maarufu wenye
ushawishi duniani na Mabalozi wa hiari wa Utalii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...