Katibu mkuu huyo wa Chama cha Mapinduzi CCM, Komredi Daniel Chongolo ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ilala.
Amesema kama yalivyo makundi mengine katika Jamii, nalo kundi hilo ni Muhimu kwa Ustawi hivyo haliwezi kuachwa nyuma kwa Sababu limekuwa likitegemea kuendesha maisha yao na kujipatia kipato halali kupitia kupitia kazi hiyo.
"Ndugu zangu labda niwaambie kuwa Jamii ya Waendesha Bajaj na Boda boda ni kundi muhimu kwenye Jamii, kwa hiyo niwasihi sana tuache kutoa taarifa zenye mrengo wa kupotosha umma kwamba kundi hilo litaondoshwa kufanya kazi zake maeneo ya katikati ya Mji" amesema Chongolo.
Amesema hatua ya sasa inayofanyika ni zoezi la kuwaratibu ili kuwawekea vituo rasmi vya Kuwatambulisha kwa Watu wanaotaka kutumia aina hiyo ya Usafiri na Sio kuwazuia kufika mjini.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo wa CCM ametaka kuheshimiwa kwa kundi la Waendesha Bajaj Wenye Ulemavu, akieleza ni kundi muhimu linalopata mkopo wa Asilimia 10 unaotolewa na halmashauri, hivyo watengewe maeneo yao ili kuepuka kugombea Abiria na Waendesha Bajaj Wasiokuwa na Ulemavu.
Wakati huo huo Chongolo ametumia mkutano huo kuwakumbusha majukumu wajumbe wa kamati za siasa za ngazi zote wakiwemo viongozi wa Jumuiya ya Chama hicho, ambao kwa sasa kwa tathimini iliyopo Kamati hizo hazitekelezi majukumu sawasawa hasa kusimamia ajenda za Wananchi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akihutubia Wajumbe wa Halmashauri Kuu Maalum ya CCM Wilaya ya Ilala katika ukumbi wa Arnatoglo, Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.(Picha na CCM Makao Makuu)
Pichani sehemu ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dar Es Salaam walioshiriki Kikao cha Halmashauri Kuu Maalum ya CCM Wilaya ya Ilala ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Arnatoglo, Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.(Picha na CCM Makao Makuu)
Pichani sehemu ya Wajumbe waliohudhuria Kikao cha Halmashauri Kuu Maalum ya CCM Wilaya ya Ilala ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Arnatoglo, Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.(Picha na CCM Makao Makuu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...