Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndugu Christina Mndeme amewahimiza wakazi wa Shina namba 2, Tawi la Mapinduzi kujisajili kwenye kadi mpya za Chama Cha Mapinduzi za Kielektroniki ambazo pia zinaweza kutumika kuwekea pesa na kufanya manunuzi katika baadhi maduka na kutumika kama kadi ya kuingilia kwenye viwanja vya michezo.
“Kwanza ni rahisi kuibeba lakini pia kadi hii unaweza kuiwekea hela kama unavyoweka kwenye simu ukipenda, na unaweza kwenda kwenye baadhi ya maduka ukaitumia hii kadi kununua bidhaa”
Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) ameyasema hayo mara baada ya kushiriki uchaguzi wa Viongozi wa Shina namba 2, Tawi la Mapinduzi, Mtaa wa Vikonje B, Dodoma.
Pamoja na mambo mengine Ndugu Mndeme amewataka Vijana kutobaki nyuma katika chaguzi hizi za ndani ya Chama cha Mapinduzi, na pia amepongeza Wakazi wenzake wa Shina namba 2 kwa kuchagua Viongozi kwa kuzingatia taratibu, Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, Miongozo na Kanuni.
Naibu Katibu Mkuu Ndeme ameutaka Uongozi mpya wa Shina namba 2 kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo nchini.
Kwa upande mwingine Diwani wa Kata ya Mtumba Mwalimu Mstaafu Edward Maboje amehimiza wananchi kuendelea kujenga shule ya Vikonje ili kuepusha watoto kwenda umbali mrefu.
Katika Uchaguzi huo Ndugu Edward Mgogodi Nghuku aliibuka mshidi kwa kupata kura 29, dhidi ya Ndugu Nasoni Mgogodi Nghuku aliyepata kura 2, na kura 5 ziliharibika.
Shina namba 2 lina wanachama 63, na waliojitokeza kwenye uchaguzi ni wanachama 36.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndugu Christina Mndeme akitoa elimu juu ya kadi za kieletroniki na umuhimu wake kwa wanachama wa CCM mara baada ya kupiga kura na kuchagua Uongozi wa Shina namba 2, Tawi la Mapinduzi, Mtaa wa Vikonje B, Dodoma. (Picha na Adam H. Mzee/ CCM Makao Makuu)


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndugu Christina Mndeme akipiga kura ya kuchagua Uongozi wa Shina namba 2, Tawi la Mapinduzi, Mtaa wa Vikonje B, Dodoma. (Picha na Adam H. Mzee/ CCM Makao Makuu)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...