Na Amiri Kilagalila,Njombe
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu ametuma salamu
za pole kwa wafiwa kutokana na vifo vya watu 9 waliofariki kwa ajali ya
gari mkoani Njombe.
Akitoa salamu hizo kwa niaba ya Rais katika
ibada ya kuaga miili hiyo katika kanisa la mtakatifu Joseph jimbo
Katoliki Njombe mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba ametoa wito kwa
waombolezaji kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.
“Lakini
pia napenda kuchukua nafasi hii kutoa salamu za pole kutoka kwa Rais wa
jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye naye
ameguswa sana na msiba huu”alisema Waziri Kindamba.
Kwa upande
wake mhashamu Askofu John Chrisostom Ndimbo wa jimbo Katoliki la Mbinga
na msimamizi wa kitume wa jimbo katoliki la Njombe ametoa shukrani kwa
serikali,jeshi la polisi pamoja na madaktari kutokana na ushirikiano
mkubwa waliouonyesha katika kipindi hiki kigumu kwao.
“Nikushukuru
mkuu wa mkoa ulikuwa mstari wa mbele kwa niaba ya serikali ya Tanzania
uliposkia taarifa za ajali hiyo,ukakimbia mahospitalini kuwaona lakini
pia ukakimbia katika sehemu ya ajali”alisema mhashamu Askofu John
Chrisostom Ndimbo
Watu hao ambao ni kutoka umoja wa vijana
Katoliki Njombe (UVIKANJO) walifariki kwa ajali ya gari tarehe 24 katika
eneo la Igima kibaoni walipokuwa wakitoka
kutembelea kituo cha kulea watoto yatima kilichopo Ibumila wilayani Njombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...