Saa
chache kabla ya kuzinduliwa rasmi filamu ya Royal Tour ya Tanzania
tayari mwanga na manufaa yake yameanza kuonekana ambapo wafanyabiashara
na watu wengine mashuhuri walioona vipande vya awali vya filamu hiyo na
kuvutiwa leo wamekutana na Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika
mkutano huo uliofanyika kwenye klabu ya faragha ya Lotos hapa New York,
miongoni mwa waliohudhuria ni Meya mashuhuri wa jiji la New York, Eric
Adams, ambaye ameeleza kuipenda Tanzania na kuahidi kuitangaza zaidi
katika jiji lake la New York.
Mtu mwingine mashuhuri
aliyehudhuria ukiondoa mabilionea na wamiliki wa makampuni makubwa
duniani ikiwemo watangazaji wa CNN, CBS nk alikuwa ni Gayle King
mtangazaji mashuhuri wa vipindi vya CBC Mornings na “King in the House”
Gayle
kwa hapa Marekani ni mtu mashuhuri akijulikana pia kwa urafiki wake wa
karibu na wa miaka mingi na nguli mwingine Oprah ambako pia yeye Gayle
ni Mhariri wa jarida la Oprah la O Magazine!
Jioni hii na usiku wa manane kwa saa za Tanzania, Rais Samia ataizindua filamu hiyo katika ukumbi wa Guggenheim Museum New York.Source: Diaspora News!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...