Na Mwandishi Wetu Tanga,

WAKALA wa Barabara Nchini (Tanroads) Mkoa wa Tanga  imezitaka taasisi zilizokuwa na miundombinu  kwenye eneo la mradi wa barabara ya Tanga Pangani kuhakikisha inaondolewa kwa wakati ili kumuondolea vikwazo mkandarasi aliyeko saiti kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo.

Taasisi hizo ni pamoja na shirika la umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Tanga, mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga (Tanga Uwasa)  pamoja na kampuni za mawasiliano ikiwemo TTCLna Halotel ambazo miundombinu yake imepita kwenye eneo hilo la barabara.

Wito huo umetolewa na Meneja wa Tanroad Mkoani Tanga Mhandisi Eliazary Rweikiza wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani.

Alisema barabara hiyo itakapokamilika itasaidia kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa Mkoa wa Tanga na wilaya itakayofikiwa na barabara hiyo.

Meneja Rweikiza amesema ni vyema taasisi hizo zikahakikisha wanaharakisha kutoa miundombinu yao katika barabara hiyo ili kumuwezesha mkandarasi kumaliza ndani ya muda aliopewa.

Hata hivyo amekemea watu wenye tabia za kuharibu miundombinu ya barabara mkoani humo kuacha mara moja tabia hiyo kabla hawajachukuliwa hatua kali za kisheria.

Meneja huyo amesema kwamba Serikali inatumia gharama kubwa kuweza kutengeneza barabara hizo hivyo hawawezi kuona watu wanaziharibu na kuwafumbia macho.

Aidha aliwasihi wananchi kuacha kuharibu miundombinu hiyo kwani inafaida kubwa kwa wananchi hivyo wahakikisha wanailinda na kuitunza ili iweze kuendelea kuwepo kwa vizazi vya sasa na vijavyo huku akieleza watakaobainika kufanya uharibifu watachukuliwa hatua kali za kisheria.

"Tutahakikisha tunashirikiana na Serikali ya mkoa ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama kuwashughulikia kwani hairuhusiw kuiba au kuharibu miundombinu ya barabara kutokana na kwamba fedha nyingi zinatumika kwenye ujenzi wake “Alisema Meneja huyo wa Tanroad Mhandisi Rweikiza.

Meneja wa Wakala wa Barabara mkoani Tanga, Eng Eliazary Rweikiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...