Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Kilimanjaro

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Tanzania Bara Abdulrahman Kinana amesema amefurahishwa na ushirikiano uliopo kati ya viongozi wa Chama na Serikali katika Mkoa wa Kilimanjaro ambao umekuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza kwenye kikao kazi cha ndani kwa wanachama wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro leo Aprili 26, mwaka 2022, Kinana amesema amesikiliza taariza zote mbili za Chama na Serikali , zimethibitisha ushirikiano uliopo kwa viongozi wote katika kusimamia maendeleo.

“Niwapongeze kwa ushirikiano kati ya Serikali na Chama, viongozi wa Chama na Serikali wa Mkoa wanafanya kazi pamoja, nahakika na wilayani ni hivyo hivyo mnatembea pamoja.Mnashiriki shughuli za maendeleo pamoja, pale ambapo Serikali na Chama mnashirikiana hata maendeleo ya wananchi yanapatikana kwa urahisi na zaidi ya hapo hata migogoro huwa imepungua, hivyo nawapongeza wote kwa ushirikiano huu,”amesma Kinana.

Aidha amewapongeza kwa kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kila sekta na mafanikio hayo msingi wake ni umoja na kujitathimini.Ni dhahiri bila fedha hakuna maendeleo, niishukuru Serikali ya CCM kwa kuleta fedha nyingi mkoani Kilimanjaro ambazo zimesaidia kuleta maendeleo.

Kwa upande mwingine, Makamu Mwenyekiti wa CCM amewakumbusha wanachama wa Chama hicho kuhakikisha katika uchaguzi wa ndani viongozi watakaopatikana wasiwe wanaotokana na rushwa bali wawe wanatokana kwa sifa za uongozi katika kukitumikia Chama na wananchi.

Amesema CCM imekaa madarakani muda mrefu kwasababu nyingi sana lakini sababu kubwa kila mtu ana uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa,hivyo wakiharibu uhuru kwa wanachama kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa nguvu ya Chama hicho itapungua.

“Mtu atakuwa na sifa za uongozi lakini hataki kugombea kwasababu kuna mizengwe mingi na rushwa.Tunaka mtu aseme akigombea atagombea kwa haki na akishinda atashinda kwa haki, ikifika mahali mtu ananunua uongozi ujue amefilisika.

“Msiruhusu watu kununua ongozi kwa kutoa rupia, kataeni na niwaambie katika kipindi cha kuelekea uchaguzi ndani ya Chama kuna watu walikuwa hawawajui kwa kipindi chote lakini sasa hivi wanaanza kuwasalimia,watakuwa wanapitisha bahasha.

“Kataeni , mtu akinunua uongozi huo uongozi utakuwa ni wake sio wenu, lakini mkimpa kura kwa njia halali basi uongozi ni wenu , atawasikiliza.Lakini pia kuna watu wakati wa uchaguzi wanapenda kuchafua wenzao, wanazua mambo yasiyokuwepo.Watu wanaochafua wenzao msiwape nafasi ya kuwasikiliza,”amesema Kinana.

Ameongeza rusha katika uchaguzi imesababisha wapiga kura hata wakipewa CV ya mgombea hakuna anayehangaika kuisoma , bali wanasubiri kupata bahasha ya kaki ambayo ndani itakuwa na noti, jambo ambalo si vizuri na vema likakomeshwa.

“Kwa hiyo na ninyi msiendekeze, niwaombe viongozi mtende haki na tunataka kiongozi ambaye watu wanamhitaji, kuna viongozi vizuri lakini wanaogopa kugombea kwasababu uwepo wa kashkash, wananchi wanampenda, viongozi wa ccm wanamtaka.

“Tunataka kuwa na viongozi wakienda mbele ya wananchi wanakubalika, kwa hiyo nitoe rai hakikisheni tunatenda haki.Mtu akileta CV yake pokea na akileta bahasha yake mwambie hili ni tatizo, najua mnacheka kwasababu inataka roho mtakatifu akushukie ili ukatae hiyo bahasha.Niwaombe tukatae rushwa katika chaguzi zetu.”


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Tanzania Bara,Ndugu Abdulrahman Kinana akiteta jambo na mmoja wa Wanachama wa CCM,mara baada ya kumaliza kikao chao cha ndani katika ukumbi wa CCM mkoa Kilimanjaro leo Aprili 25,2022.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...