



Wananafunzi wa za Sekondari Zanaki na Kibasila wakiwa kwenye maeneo mbalimbali ya Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini wakati wa zira yao ya mafunzo Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV )
*Wapongeza DAWASA kwa kazi kubwa usambazaji wa maji Safi na Salama
Na Emmanuel Massaka,Michuzi TV
WANAFUNZI wa Klabu za Maji na Usafi wa Mazingira kutoka shule za Sekondari Zanaki na Kibasila jijini Dar es salaam zimefanya ziara ya mafunzo katika Mtambo wa uzalishaji maji Ruvu Chini ikiwa kutrngeneza sehemu ya mabalozi katika kuelimisha jamii juu shughuli za Uhifadhi na utunzaji wa Miundombinu ya maji.
Klabu za wanafunzi husimamiwa na kuendeshwa na DAWASA katika kuwaandaa wanafunzi hao katika kuthamini umuhimu wa maji na kuelimisha wazazi wao namna bora kutuza maji.
Akizungumza na wanafunzi wa shule hizo Meneja wa Mtambo wa Uzalishaji wa Maji Ruvu chini, Immakulata Msilama amewasihi wanafunzi kutunza vyanzo vya maji na kuepukana na kufanya shughuli za kibidamu katika vyanzo hivyo.
Amesema maji wanayayoa kwenye Mto Ruvu Kuzaliza maji hayo kuna gharama za dawa katika kuchakata maji hayo kuwa safi na salama.
Emmaculata amesema kuwa kadili ya maji yanavyokuwa machafu gharama za uchakataji maji zinaongezeka uzalishaji.
Amesema amefurahishwa na wanafunzi wa Klabu kufika katika Mtambo kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Zanaki,Upendo Kibaki amewapongeza Dawasa kwa namna wanavyozalisha maji kwa wingi na kusambaza kwa wananchi na kufanyika maendeleo mbilimbali katika jiji la Dar es Salaam.
Kibaki amewaomba wanamchi kuvitunza vyanzo vya maji na maundombinu yake ambayo yanasambazwa na DAWASA
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Zanaki,Aisha Lyavo amesema atahakikisha wanakwenda kutoa elimu kwa wananchi wa maeneo mbalimbali kuhusiana na utuzaji wa vyanzo vya maji pamoja na miundombinu ya mitambo na mabomba.
Kwa upande wake Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibasila,Dhul-Kifili Abubakari ameshangazwa na kazi kubwa inayofanywa na DAWASA ya kuzaliza maji kwa kupitia mitambo ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.
"Nilichokiona leo kimenishangaza sana sikuwahi kufahamu kuwa DAWASA wana kazi kubwa ya ya kulinda wananchi kwa kuwapatia maji safi na salama".amesema Mwanafunzi Dhul-Kifili
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...