Na Humphrey Shao,Michuzi Tv
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022, Sahili Geraruma ameonesha kusikitishwa na hali ya udanganyifu wa nyaraka na dharau katika ujenzi wa Zahanati ya Kawe wilayani Kinondoni mkoa wa Dar es Salaam , hivyo kuamua kutoweka jiwe la msingi katika mradi huo.
Akizungumza mara baada ya kupitia nyaraka za Manunuzi kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 ametoa tuhuma hizo na kisha kuwaba radhi wakazi wa Kawe baada ya kuchelewa kutoka ndani kwasababu ya ugumu wa nyaraka zilizowassilishwa katika eneo hilo.
Akielezea zaidi amesema “Kwanza viongozi wa manunuzi wa eneo hilo wameonyesha dharau kubwa kwani licha ya kutangaza jukwaani Kuwa wakifika kwenye mradi wakute nyaraka lakini bado wameonesha ukaidi.”
Ameongeza pili kumekuwa na udanganyifu katika Manunuzi ya Vigae (Tiles) ambazo zilitakiwa kuwekwa na kuwekwa saizi nyingine.
Kwa mujibu wa Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge kitaifa amesema kwa upande wa Manunuzi umefanya udanganyifu wa nyaraka za ununuzi wa nondo ambazo certificate zake ni za mradi wa madarasa ya Uviko 19 wakati kinachojengwa ni Zahanati.
Kutokana na tuhuma hizo za ufanganyifu wa nyaraka ameamua kutoweka jiwe la msingi katika Zahanati hiyo na kuagiza Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kufanya ukaguzi ndani ya siku tatu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Godwin Gondwe akipokea Mwenge kutoka kwa Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam , Hassan Abbas Lugwa katika Viwanja vya Bunju A Kinondoni.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni,Khanifa Suleiman Hamza akitoa maelezo Kwa mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru 2022
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wakipitia nyaraka za mradi neno Kwa neno wakati wa kukimbizwa Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Kinondoni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Godwin Gondwe akikabidhi Lisala ya Utii Kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Sahil Geraruma mara baada ya kukagua miradi yote
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...