Mwenyekiti wa Makampuni ya Supedoll, Seif Seif (wa tatu kulia) akizungumza jambo na Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam, Prof. William Anangisye (wa pili kulia) aliyetembelea Kampuni ya Superdoll, iliyopo Barabara ya Pugu, jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na ujumbe wake walifanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho kwa lengo la kuona uwekezaji wa kampuni hiyo pamoja na kuangalia namna nzuri ya kushirikiana.  Kulia ni Meneja Mkuu wa Superdoll, Ibrahim Juma.
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam, Prof. William Anangisye akifafanua jambo kwa Uongozi wa Kampuni ya Superdoll, katika kikao chao kilichofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo, iliyopo Barabara ya Pugu, jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Prof. Benadetha Kilian.
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam, Prof. William Anangisye akimueleza jambo Mwenyekiti wa Makampuni ya Supedoll, Seif Seif wakati wakiwa kwenye ziara ya kutembelea sehemu ya vitengo vya Kampuni hiyo, iliyopo Barabara ya Pugu, jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...