HUKUMU ya dhidi ya kesi ya kusambaza picha za ngono mtandaoni inayomkabili mtangazaji wa Clouds fm, Burton Mwemba maararu kama Mwijaku inatarajia kusomwa Mei 31,2022 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mwijaku anakabiliwa na kesi ya kusambaza picha za utupu mtandaoni kesi inayounguruma mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rhoda Ngimilanga.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya mshtakiwa Mwijaku leo Mei 11, 2022 kumaliza kujitetea pamoja na mashahidi wake watatu aliowaleta Mahakamani hapo.
Mapema, Mei 2 mwaka huu, Mwijaku alikutwa na na kesi ya kujibu wakati kesi hiyo ilipoletwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi kama anakesi ya kujibu au la, baada ya upande wa mashtaka kumaliza kutoa ushahidi wao.
Baada ya kutolewa uamuzi huo, Mwijaku aliieleza mahakama kwamba atakuwa na mashahidi watatu wakati akitoa utetezi wake.
Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi watano pamoja na vielelezo vinne.
Mwijaku anakabiliwa na kesi ya kusambaza picha za utupu mtandaoni kinyume cha sheria.
Inadaiwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo katika terehe tofauti kati ya Septemba 17 hadi Oktoba 10 mwaka 2019 jijini Da r es Salaam ambapo anadaiwa wa kusambaza picha za utupu akitumia kompyuta yake kupitia mtandao wa WhatsApp.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...