Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuanza kusikiliza utetezi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kufuatia mawakili kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) wanaoendesha kesi hiyo kushindwa kufika mahakamani hapo.

Wakili wa serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Nickson Shayo amedai mbele ya Hakimu Mkazi Evodia Kyaruzi amedai leo Mei 17, 2022 kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya mshtakiwa Maimu kuanza kujitetea.

Amedai wamekuwa wakiendesha kesi hiyo kwa ushirikiano na mawakili kutoka ofisi ya DPP ambao wameshindwa kufika leo mahakamani hivyo, ameomba mahakama iahirishe kesi hiyo hadi tarehe nyingine.

Wakili wa utetezi, Kung'he Wabeya hakuwa na pingamizi juu ya ombi hilo akidai kuwa alipigiwa simu na Wakili wa Serikali, Ladislaus Komanya na kumueleza kuwa hawataweza kufika mahakamani kwakuwa wamepewa kazi maalum.

Kutokana na hali hiyo mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Mei 31 mwaka huu.

Washitakiwa wote wameieleza mahakama kuwa, katika utetezi wao watakuwa na mashahidi pamoja na vielelezo mbalimbali huku Maimu akieleza kuwa atakuwa na mashahidi sio chini ya 20 pamoja na vielelezo visivyozidi 10.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na jumla ya mashahidi 26 pamoja na vielelezo 45.

Mbali ya Maimu na washitakiwa wengine ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Sheria Sajina Raymon, Xavery Kayombo Meneja Biashara wa (NIDA), Aveln Momburi, na George Ntalima.

Maimu na wenzake wanakabiliwa na mashitaka mbalimbali likiwemo kuisababishia hasara serikali Sh bilioni 1.175.

Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 55 likiwemo la aw genge la uhalifu, kugushi, kutoa nyaraka za kugushi kwa lengo la kumdanganya mwajili, kusababisha hasara, utakatishaji fedha na Matumizi mabaya ya madaraka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...