KADA WA Chama cha Mapinduzi(CCM) Venance Mwamoto amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua yake ya kupandisha mishahara ya wafanyakazi nchini na hali iliyopelekea kumaliza kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi nchini.

Mwamoto ambaye pia ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kilolo amesema hayo leo, siku chache hatua ya Rais Samia kuridhia mapendekezo ya mishahara ikiwemo kima cha chini Kwa watumishi wa umma kwa asilimia 23.3.

Hatua hiyo ya Rais Samia ni utekelezaji wa ahadi aliyokuwa ameitoa wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani ambapo pamoja na mambo mengine, aliahidi kuongeza kima cha mishahara kwa wafanyakazi Jambo ambalo lilikuwa kilio chao kwa muda mrefu.

"Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa hili anastahili pongezi nyingi Sana, amedhirisha wazi wazi kuwa yeye ni mama mwenye malezi mazuri na ujali kwa wanae, madai ya nyongeza ya mishahara ilikuwa kilio cha miaka mingi hapa nchini, kwetu sisi" amesema Mwamoto.

Aidha kupitia taarifa hiyo iliyotolewa na Ikulu, nyongeza hiyo ya mishahara imefanyika kwa kuzingatia Pato la Taifa (GDP), mapato ya ndani yanayotarajiwa kukusanywa mwaka 2022/2023 na Hali ya uchumi wa ndani na nje ya nchi.

Kutokana na hatua hiyo, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imepanga kutumia kiasi cha Sh Trilioni 9.7 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishahara ya watumishi wote katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na Wakala za Serikali.

Hivyo kwa hatua hiyo bajeti ya Serikali ya Mwaka 2022/2023 ina ongezeko la Sh Trilioni 1.59 sawa na asilimia 19.51 ikilinganishwa na bajeti ya Mwaka 2021/2022.

Alisisitiza kwa kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi siku zote kimekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha maslahi ya wananchi wake yanasimamiwa na kulindwa hatua iliyomfanya Rais Samia kuwa kiongozi bora kila kukicha.














Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...