Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akifurahia ambo wakati akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD FDD Ndugu Ntakarutimana Joseph mara baada ya kuwasili Mugina mkoani Makamba, Burundi.Katibu Mkuu ameongozana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdullah Juma Saadallah pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga kwa ziara ya kuimarisha uhusiano wa vyama hivyo viwili pamoja na kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa uwanja wa kisasa wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex zitakazofanyika tarehe 25, Juni 2022 Makamba nchini Burundi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwapungia wananchi mara baada ya kuwasili Mugina mkoani Makamba, Burundi leo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipiga ngoma ya wenyeji wa Burundi mara baada ya kuwasili Mugina mkoani Makamba, Burundi.
Katibu Mkuu ameongozana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdullah Juma Saadallah pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga na kupokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama cha CNDD FDD Ndugu Ntakarutimana Joseph.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...