Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imeingia Mkataba wa Ushirikiano katika Utendaji Kazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP Tanzania).
Mkataba huo unalenga ushirikiano katika kuimarisha utekelezaji endelevu katika Ununuzi wa Umma (Improving sustainable public procurement practices).
Mkataba huo umesainiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Bw. Eliakim Maswi na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, Bi. Christina Musisi.
Wengine waliokuwa wameongozana na Afisa Mtendaji Mkuu katika tukio hilo lililofanyika Jijini Dar es Salaam ni Kaimu Mkurugenzi wa Kujenga Uwezo na Huduma za Ushauri, Bw. Castor Komba, Mkuu wa Kitengo Cha Ununuzi, Bw. Robert Kitalala, Kaimu Meneja wa Mahusiano kwa Umma Bw. Mcharo Mrutu na Afisa Mipango Mkuu Bw. Martin Sapanjo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Bw. Eliakim Maswi na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, Bi. Christina Musisi kwa pamoja wakitia saini Mkataba wa Ushirikiano katika Utendaji Kazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP Tanzania) leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Bw. Eliakim Maswi na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, Bi. Christina Musisi kwa pamoja wakionesha nyaraka za Mkataba wa Ushirikiano katika Utendaji Kazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP Tanzania) mara baada ya kusaini leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...