Na .WAF-Dodoma

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo June 24,2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Zabulon Yoti kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu Afya.

Miongoni mwa mambo walioyajadili ni pamoja na uzinduzi wa utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 katika Mkoa wa Manyara ambapo watashiriki viongozi kutoka Wizara ya Afya pamoja na Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika la Afya Duniani na wananchi kwa ujumla.

Aidha Dkt. Yoti ameahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kupambana na ugonjwa wa Polio na UVIKO-19 pamoja na kutoa ushauri Serikali iendelee kuhuisha mara kwa mara Mpango Mkakati wa utoaji wa chanjo nchini.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...