WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kufanya mazungumzo na makamu wa Rais na meneja mkuu wa Paramount Africa and Peer Lead BET International, Monde Twala, na kukubaliana kushirikiana katika kuiwezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa tuzo za MAMA- MTV Africa Music Award kwa mwaka 2023.
Waziri
Mchengerwa amekutana na Monde Twala Jijini Los Angeles katika jimbo
la California nchini Marekani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za BET kwa
mwaka 2022.
Katika mazungumzo
hayo Waziri Mchengerwa amemwelezea nia na sababu ya Tanzania kutaka kuwa
mwenyeji wa tamasha hilo la utoaji wa tuzo hizo kubwa za burudani kwa
Afrika, kuwa ni kuongeza ushawishi kwa vijana wa kitanzania kuendelea
kufanya vizuri katika sekta za burudani Pamoja na kuitangaza zaidi
Tanzania na uzuri wake katika ulimwengu.
Katika
mazungumzo hayo pande zote mbili zimekubaliana kuungana kwenye
kutafuta washirika katika kuendesha tuzo hizo, na kuridhia kuwa
maandalizi yaanze mara moja, huku wakipendekeza muda wa tamasha hilo la
utoaji tuzo kufanyika mwezi Octoba 2023 jijini Dar Es Salaam.
“Tuna
kila sababu ya kuwa mwenyeji wa Tuzo za MAMA- MTV African Music Awards
kwa mwaka 2023 kwa sababu lengo letu ni kuitangaza nchi yetu zaidi na
katika hili lazima tufanikiwe, kwa sababu hakuna kinacho shindikana,
tuna kila kitu na ninaamini tunaweza” alisema Waziri Mchengerwa.
Kwa
upande wake Tawla amesema anaiona Tanzania kama eneo lenye vipaji vya
hali ya juu katika sekta ya Sanaa, na burudani ambavyo havijaonekana na
kutumika kwa manufaa ya nchi na manufaa ya wasanii wenyewe, na kuahidi
kushiriki moja kwa moja katika kuwezesha kufanyika kwa tuzo hizo nchini
Tanzania kwa mwaka 2023.
Katika
ziara hiyo Waziri Mchenegerwa ameambatana na Katibu Mkuu Dkt. Hassan
Abbasi pamoja na Mkurugenzi wa Sanaa dkt. Emmanuel Ishengoma ambao wapo
nchini marekani, kutafuta uzoefu wa namna ya kuandaa tuzo kwa kiwango
cha kimataifa, lengo likiwa ni kuunga mkono juhudu za Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuitangaza
Tanzania kimataifa kupitia washiriki wa moja kwa moja na mamilioni
watakao fuatilia mubashara tamasha la utoaji wa tuzo hizo.
Wakiwa
Nchini Marekeni wameudhuria tamasha la utoaji wa tuzo za BET kwa mwaka
2022, lililofanyika June 26 katika ukumbi wa burudani (arena) wa
Microsoft theater, tuzo ambazo ni za kimataifa zinazotolewa mara moja
kwa mwaka kama sehemu ya kusherehekea mafaniko ya wamarekani weusi
katika muziki, maigizo na michezo.
Viongozi
hao pia wanatarajia kutembelea kampuni mbalimbali za uzalishaji wa
filamu na muziki, lengo likiwa ni kutengeneza mahusiano na kuona namna
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inavyoweza kuwawezesha wataalamu
kutoka katika makapuni hayo maarufu duniani kuwajengea uwezo wazalishaji
wa muziki na filamu wa hapa nchini Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...