Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh.Anthony Mtaka akizungumza wakati wa kuzindua kampeni ya badili tabia Sepesha Rushwa itakayo tekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu Katika mikoa ya Dodoma, Dar Es Salaam na Arusha na amewasihi wanafunzi kuwa mstari wa mbele kukomesha vitendo vya Rushwa hapa nchini.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU DODOMA-Victor Swella akizungumza wakati wa kuzindua kampeni ya badili tabia Sepesha Rushwa itakayo tekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu Katika mikoa ya Dodoma, Dar Es Salaam.


Baadhi ya Wanafunzi wa vyuo vikuu mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye maandamano ya kupinga vitendo vya Rushwa.

Na Janeth Raphael - Dodoma DODOMA
TAASISI ya Sauti ya wapinga rushwa nchini (ACVF) imezindua kampeni ya badili tabia sepesha rushwa itakayo tekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu Katika mikoa ya Dodoma, Dar Es Salaam na Arusha kwa lengo la kusaidia harakati za kuzuia vitendo vya rushwa.

Akizungumza kwenye uzinduzi Jijini Dodoma ,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amietaka Taasisi hiyo kufanya kazi kwa malengo yaliyokusudiwa ili kukomesha vitendo vya rushwa.

"Nimefurahi mno kuona kuna watu bado hawalali wanaendeleza mapambano ya rushwa,nani asiyependa kuona rushwa inatokomezwa!niwaahidi kwa nafasi yangu nitafanya mkutano mkubwa na kuwashirikisha club zote za wapinga rushwa wote wa shule ya msingi hadi vyuoni hii itasaidia kutengeneza mabalozi wa rushwa kwa Kila maeneo ambao Serikali imepeleka fedha za miradi." Amesema

Mtaka amesema Serikali inataka kuona kunakuwa na mabalozi wapinga rushwa hadi vyuoni kwa sababu miradi mingi mikubwa imekuwa ikitekelezwa hapa nchini haikidhi vigezo vinavyotakiwa kutokana na baadhi ya wengine kutokuwa waaminifu kwenye fedha za umma.

"Tunaposepesha rushwa lazima tuone umuhimu wa kuingia kiundani zaidi ili tusepeshe kiukweli, tusipoongeza juhudi hata miradi yetu mikubwa inayofanyika hapa nchini itashindwa kukamilika ipasavyo." Amesisitiza

Mbali na hayo amesisitiza kuwa Ofisi yake kwa kushirikiana na ACVF wataandaa Mpango wa kutoa uhamasishaji wa elimu ya rushwa kwenye michezo ya umiseta na ngazi ya mikoa kutakuwa na mashindano ya michezo ili kila mmoja aone rushwa ni kuti kibaya.

"Tukifanya yote haya Jamii itakubali kuondoa mambo ya hovyo ikiwemo rushwa ya ngono lazima tuwawajibishe ,tusirithishe ujinga watoto wetu aina hii ya ujinga haitajirudia kwa vizazi vijavyo na kama tuna watu badó wanawaza kurubuni watu kwa rushwa hiyo ni aina fulani ya ujinga." Amesema

Naye Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Victor Swella amesema Ofisi hiyo itashirikiana na ACVF kutoa elimu kwenye makundi mbalimbali na kuleta umaana kwenye mapambano haya.

Amesema lazima kuwe na mipango mizuri ya kuratibu namna ya kutoa elimu ili kuwafikia watu wote kwa urahisi ikiwa ni Pamoja na akuwafuata kwenye mitaa na minadani kufikisha ujumbe huu.

"Tupeleke zaidi elimu kwa watu wa chini ambao wananyimwa haki yao Kwa sababu ya rushwa, Kuna wengine hata hawajui viashiria vya rushwa ni kazi yetu kuwaelimisha bila kuchoka ili Kila mtu aishi kwa amani na utulivu. "Amesisitiza

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Mabolozi wa Sauti ya wapinga rushwa (ACVF) Kubega Dominic amaesema Kampeni ya Badili tabia, Sepesha Rushwa ilizinduliwa mnamo tarehe 01 Mei 2022, jijini Dar es Salaam Chini ya Afisa Wa dawati la elimu Kwa umma TAKUKURU Mkoa Wa Kinondoni, Bibie Msumi ikiwa ni ndiyo mwendelezo Wa Kampeni iliyozinduliwa Dodoma.

Amesema Kampeni hiyo inashika Kasi na Kufanya Vema kwenye Mitandao ya Kijamii Kupitia Kurasa za Facebook, Instagram,Twitter, Linked in, Google Business na YouTube na kwamba mara baada ya uzinduzi Wa Kampeni hiyo wamefanikiwa Kuandaa na kushiriki Matukio mbalimbali Ngazi za Kanda.

"Tumeushiriki mdahalo Wa Jumuiya ya Wapinga Rushwa uliofanyika tarehe 13 Mei 2022 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Chini ya Wanafunzi wa kitivo cha Falsafa na Maadili na Kongamano la Maazimisho ya Miaka 15 ya kuanzishwa Kwa Jumuiya za Wapinga Rushwa Vyuoni nchini Tanzania, lililofanyika tarehe 14 Mei 2022." Amesema

Amesema ACVF ikiwa ni Taasisi inayolenga kuongeza ufahamu juu ya Rushwa ngazi ya Kitaifa wataendelea kupaza sauti na harakati za Kupambana na kuzuia rushwa nchini Kwa kauli Moja ya BADILI TABIA #SEPESHARUSHWA

"Kwa kubaini hayo ACVF tuliamua kusimama Vema na kuamini kuwa sababu kubwa inayopelekea kuendelea kushamiri vitendo vya Rushwa ni TABIA, na hilo ndilo chimbuko la kauli hii tunayotumia kuhamasisha jamii isemayo BADILI TABIA #SepeshaRushwa ili kutokomeza Rushwa LAZIMA kubadili tabia."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...