Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde akiteta jambo na mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda Cha mbolea Nala jijini Dodoma Nduwimana Nazaire.
Naibu Waziri Mavunde pamoja na Wabunge wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda Cha mbolea Nala jijini Dodoma.
Naibu Waziri Mavunde pamoja na Wabunge Kutoka nyanda za Juu kusini katika ziara ya kutembelea Kiwanda Cha mbolea ITRACOM kilichopo Nala, jijini Dodoma
SERIKALI imewaelekeza taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini (TARI), Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) na Itracom, kuhakikisha wanapitia Kanda za Ikolojia nchi nzima sambamba na kupima afya ya udongo ili mbolea itakayozalishwa iendana na mahitaji ya udongo wa eneo husika.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde wakati wa ziara ya Wabunge wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inayozalisha vyakula kwa wingi hapa nchini,walipotembelea kiwandani hapo kujua aina ya mbolea inayotarajiwa kuzalishwa mwezi ujao katika kiwanda hicho.
Mavunde amesema serikali inatambua kwamba,Nyanda za Juu Kusini ni eneo la Kiikolojia ambalo linategemewa sana kwa ajili ya uzalishaji wamazao ya Kilimo ndio maana wabunge wa maeneo hayo wamekuja kuona uzalishaji wa mbolea katia kiwanda hicho.
Naibu waziri huyo amesema kuwa sababu kubwa ya kufanya hivyo ni pamoja na kutaka kujua aina ya udongo uliopo katika maeneo tofauti hapa nchini,ili mbolea hiyo inapoanza kusambazwa iende kuleta mafanikio kwa wakulima nchini katika mazao wanayolima.
“Kabla ya kuanza uzalishaji tayari serikali ilishatoa maelekezo kwa taasisi zake husika kwenda kufanya tafiti,ikiwemo kuangalia aina ya udongo katika mikoa mbalimbali hapa nchini na kubaini mbolea aina ya Organo Mineral inayotarajia kuzalishwa kiwandani hapo inatija.”Alisema Mavunde.
Naibu Waziri alisema maeneo hayo ni ya kimkakati na ndio maana ziara hii ya wabunge kutoka Nyanda za Juu Kusini itasaidia sana kuleta uaminifu kwa wananchi lakini vilevile wataenda kuionyesha jamii jitihada ambazo zinafanywa na serikali za kukabiliana na changamoto ya mbolea hapa nchini.
Mavunde alisema uwekezaji wa kiwanda hiki ni matunda ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan na kumkaribisha muwekezaji kuja kuwekeza katika eneo hilo.
Hata hivyo alisema baada ya kupanda kwa bei ya mbolea,serikali imekuja na mkakati tofauti wa kukabiliana na changamoto hiyo na mkakati wa kwanza wa haraka ilikuwa ni kushirikisha TFRA kwa ajili ya kuhakikisha inatoa bei elekezi ili mbolea isipande bei kubwa sana kwa maeneo ambayo gharama yake halisi aiendani na uhalisia wenyewe.
Alisema TFRA walianza kutoa bei elekezi ilikuwa kama hatua ya muda mfupi, lakini hatua ya muda wa kati ilikuwa katika bajeti mpya ya serikali inayoanza Julai,serikali imedhamiria kutenga fedha kwa ajili ya Ruzuku ili kupunguza ugumu wa bei ambayo wananchi wanapata hivi sasa,iliopelekea wananchi wengi kushindwa kuhimili.
Alisema hatua ya tatu kama sehemu ya mkakati ilikuwa ni kuvutia wawekezaji kuja kujenga viwanda vingi hapa nchini,mojawapo ni kiwanda cha Itracom ambacho kinauwezo wa kuzalisha Tani 600,000 kwa mwaka.
Alisema hivi sasa mahitaji ya Samadi katika hatua ya awali ni tani 117,000 ambapo tayari wameshatengeneza vituo vya kukusanyia samadi hiyo,hivyo wafugaji watapata fursa ya kujipatia kipato kupitia mbolea inayozalishwa kiwandani hapo.
Naye Mwenyeki wa muda wa Wabunge wa Nyanda za Juu Kusini Jackson Kiswaga anaishkuru serikali kutokana na uwekezaji wa kiwanda hicho waliofanya hapa nchini.
Kiswaga alisema kama hiki kiwanda kinazalisha mbolea ya asili, basikitakuwa na faida kubwa kwa wakulima,kutokana na kwamba wakulima watapa mazao mengi.
Alisema wao kama Wabunge wa Nyanda hizo,watakwenda kuwa mabalozi wazuri katika maeneo ambayo wanatoka.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Nduwimana Nazaire aliwashkuru wabunge hao kutokana na kuwatembelea kiwandani hapo pia ameishkuru serikali kutokana na Ushirikiano inaoonyesha na kuahidi hawataiangusha serikali na mbolea wanayokwenda kuzalisha italeta matokeo chanya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...