Na. Damian Kunambi, Njombe
Mahakama ya Wilaya ya Ludewa imemhukumu kutumikia kifungo cha mika 30 jela Elisha Mkalawa (20) mkazi wa kijiji cha Ludewa mjini kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa kidato cha nne (17) ambaye jina lake limehifadhiwa.
Akisomewa hukumu hiyo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahaka ya Wilaya hiyo Isaac Ayengo imeelezwa kuwa mshtakiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi huyo na mnamo Julai 26, 2021 mwanafunzi huyo alitoroka shuleni na kwenda nyumbani kwa mshtakiwa na kukutana nae kimwili na baada ya hapo mshitakiwa alimtorosha mwanafunzi huyo kusiko julikana.
Ameeleza kuwa baada ya mwanafunzi huyo kutoonekana shuleni walitaarifiwa wazazi wake ambao nao walitoa taarifa katika kituo cha polisi na ulipo fanyika upelelezi walifanikiwa kumpata mwanafunzi huyo na baada ya kumhoji alidai mshtakiwa amempa ahadi ya kumuoa na tayari wamekwisha kutana kimwili.
Kutokana na maelezo hayo ya mwanafunzi ndipo zikafanyika jitihada za kumkamata mshtakiwa na kumfikisha mahakamani na kusomewa shitaka lake la ubakaji.
Aidha katika utetezi wake mshtakiwa huyo aliiomba mahaka imsamehe kwakuwa ana mtoto mdogo wa miezi 6, na pia wazazi wake ni wazee huku mwendesha Mashtaka Asifiwe Asajile aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na jamii kwa ujumla.
Hata hivyo hakimu Ayengo amesema amesikiliza ushahidi wa pande zote mbili na huku ushahidi wa upande wa mashtaka ukionekana kuthibitisha kosa pasipo na shaka na kupelekea mshitakiwa kutiwa hatiani hivyo mahakama inamuaru kwenda jela miaka 30 kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 130 (1) (2) (e) na 131 (1) cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 marejeo ya 2019.
.png)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...