*Yashiriki Maonesho ya Vyuo Vikuu na kutambulisha kozi ya shahada ya pili ya elimu


Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
CHUO Kikuu cha Aga Khan Tanzania (AKU) kimesema kuwa wameanzisha programu ya kutoa elimu ya afya katika jamii kutokana na kuwepo magonjwa ambayo yanatokana na kutokuwa na elimu sahihi ya kuzingatia ikiwemo ulaji wa vyakula.

Magonjwa ambayo kwa sasa yanasumbua na kushusha nguvu kazi ya taifa kama Ugonjwa wa Sukari pamoja na ugonjwa wa Shinikizo la Damu ya kupanda na kushuka.

Amesema wamebaini kuwa kufundisha pekee sio suluhisho bali wanaofundishwa masomo kwenda kutoa elimu katika jamii kuhusiana na magonjwa mbalimbali na kuamini kunaweza kupunguza idadi ya wagonjwa.

Akizungumza katika Wiki ya Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Tanzania(AKU) Dk. Eunice Siaity amesema namna Chuo kinavyotoa mafunzo kwa wanafunzi ni kwa vitendo zaidi .

Amesema Programu za elimu za elimu ya afya zinawajengea wanafunzi uwezo kwa vitendo ambapo wanashiriki kuelimisha jamii juu ya afya na lishe bora pamoja na kutoa huduma za upimaji na ushauri kwa jamii katika maeneo mbalimbali katika Mikoa ya Dar es Salaam (Kigamboni) na Mkoa wa Pwani (Kibaha).

Amesema kuwa katika maonesho hayo wameitikia wito wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza programu ambazo zinakidhi soko la ajira nchini na hivyo basi wanategemea kuongeza program za elimu na za afya.

Aidha Dk.Eunice amesema wana mategemeo ya kuanzisha shahada ya Uuguzi kwa wanafunzi wanatoka moja kwa moja shuleni kwani shahada ya uuguzi iliyopo kwa sasa ni ya wauguzi waliokuwepo kazini.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Tanzania (AKU) Dk.Eunice Siaity akizungumza na mwananchi aliyetembelea banda la Chuo hicho katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Tanzania (AKU) Dk.Eunice Siaity akiwahudumia wananchi waliotembelea banda la Chuo hicho katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Tanzania (AKU) Dk.Eunice Siaity akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa chuo hicho katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...