Kamishna wa Uhifadhi - TANAPA, William Mwakilema ameagiza Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Burigi -Chato kuboresha huduma za utalii pamoja na kuongeza juhudi za kujitangaza ili kufikia uwezo wa kujiendesha na kuchangia pato la Taifa.

Kamishna Mwakilema aliyasema hayo alipotembelea Hifadhi ya Taifa Burigi - Chato 19/07/2022 kwa lengo kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika Hifadhi hiyo.

“Boresheni bidhaa za utalii na shughuli mbalimbali za utalii na kuzitangaza zaidi ili kuchangia zaidi pato la Taifa” alisema Mwakilema.

Aidha,Mwakilema alisisitiza adhma ya serikali ya kufikia watalii millioni tano na mapato dolla za kimarekani billioni sita ifikapo 2025 na kubainisha lengo hili litatimia kwa hifadhi zote kuongeza jitihada za kujitangaza, kuongeza mazao mapya ya utalii pamoja na kuimarisha miundombinu yote hifadhini.

Kamishna Mwakilema pia ameelekeza hifadhi hiyo kuimarisha ulinzi kwa kuongeza ushirikiano na vyombo vingine vyote vya ulinzi na usalama nchini.

Akizungumza kwa niaba ya menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Burigi - Chato Mkuu wa Hifadhi hiyo Kamishna Msaidizi wa uhifadhi, John Nyamhanga

Alisema Hifadhi ya Taifa Burigi -Chato ni moja kati ya hifadhi mpya zinazoendelea kukua na tayari mikakati mbalimbali imeshawekwa kuhakikisha inaongeza bidhaa za utalii ili kuvutia wageni wengi zaidi kuitembelea.

Pia, Hifadhi imejipanga kuendelea kujitangaza katika nchi jirani kama Uganda, Burundi na Rwanda.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...