Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Celestine Mushy (kushoto)  akutana na kufanya mazungumzo na Meya wa Jiji la Linz, Mhe. Mstahiki Klaus Luger. Balozi alimshukuru kwa mapemzi yake kwa Tanzania ambayo yaliwezesha Jiji la Dodoma kuwa na mahusiano na Jiji la Linz (Sister Cities). Balozi alimuomba kuimarisha mahusiano hayo zaidi kwa kusainiana makubalino ya ushirikiano kati ya hospitali na vyuo vikuu vya Linz na Tanzania ili kuweza kubadilishana utaalamu, teknolojia, mafunzo, wanafunzi na wahadhiri. Aidha, Balozi alimuomba kuandaa mkutano wa wadau wote ili aweze kuongea nao. Mhe. Mstahiki Meya alikubali maombi hayo.

Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Celestine Mushy na Meya wa Jiji la Linz, Mhe. Mstahiki Klaus Luger wakiwa katika picha ya pamoja na wasaidizi wao baada ya kufanya mazungumzo.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...