MBUNGE wa Jimbo la Ulanga (CCM) Mhe Salim Alaudi Hasham ametatua  ya changamoto ya miaka mingi ya kukosa maji safi na salama kwa wananchi wa kijiji cha Nakafuru kata ya Lupiro wilayani Ulanga ambapo kwa sasa wakazi wake wananufaika na huduma hiyo

Wananchi hao walimuomba mbunge wa Jimbo hilo awatatulie changamoto hiyo kwani ni adha kubwa jambo linalopelekea kina mama na watoto kuteseka kufuata maji kwa umbali mrefu na wakati mwengine kunywa maji yasiyo salama jambo linalohatarisha maisha yao kwani Afya zao zinakuwa matatani.

Mbunge huyo baada ya kusikia kilio hicho akatoa kiasi cha Shilingi milioni 2.5 kwaajili ya uchimbaji wa visima vitano na utengenezaji wa miundombinu ya bomba ili maji yapatikane kwa uhakika bila changamoto.

Zoezi la uchimbaji wa visima limekamilika na mapema katibu wa mbunge wa jimbo hilo Ndugu Thomas Justice Daffa amewakabidhi wananchi visima hivyo na kuwataka wavitumie kwa umakini kwa kuvitunza ili viwasaidie kwa muda mrefu.

Visima hivyo vilivyochimbwa na kampuni ya Msabi pia vitakuwa nanutaratibu wa kufanyiwa matengenezo mara kwa mara na kampuni hiyo ili kuhakikisha wananchi wa eneo hilo hawakosi maji safi na salama wakati wote.

Baada ya kukabidhiwa visima hivyo wananchi wa eneo hilo walimshukuru mbunge kwa msaada huo mkubwa kwani kilio hicho kilikuwa cha miaka mingi na walimuomba aendelee na moyo hio wakuwasikiliza wananchi wake na kuwatatulia changamoto zao zinazowakabili.

Penye mafanikio hapakosi changamoto wanachi hao baada ya kupata maji wakaendelea kumuomba mbunge awapambanie kupata umeme wa uhakika katika baadhi ya vitongoji vyao ambavyo havijafikiwa na umeme jambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo kwani wanashindwa hata kufanya biashara ndogo ndogo kwa kukosa huduma hiyo.

Katibu wa Mbunge Ndugu Thomasi Justice Daffa kwaniaba ya mbunge aliwaahidi kulibeba swala hilo na kulisimamia kidete ili nishati hiyo muhimu iwafikie wananchi wote wa nakafuru.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...