Rais
na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akikabidhi vocha ya
dola za kimarekani 10,000 kwa Meneja Miradi ya Asasi isiyo ya Kiserikali
ya ATFGM, Valerian Mgani na Sista Jaquline Bbaga, zilizotokana na
jitihada zake za kufanikisha kukabili changamoto mbalimbali katika jamii
.
Naibu
Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa, akiongea wakati wa mkutano na
waandishi wa habari na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark
Bristow (kulia) kuhusu uwekezaji wa kampuni hiyo na jinsi inavyochangia
kkuza uchumi wa kijamii nchini.Mkutano huo pia ulihudhuriwa na viongozi
wa mkoa wa Mara na Wawakilishi wa Wananchi wa kata zilizopo jirani na
Mgodi wa North Mara.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Mark Bristow, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.
Mbunge wa Tarime, Mwita Waitara akiongea wakati wa mkutano huo uliofanyika katika mgodi wa Barrick North Mara.
Rais
na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, akikabidhi vocha ya
dola za kimarekani 10,000 kwa Meneja Miradi ya Asasi isiyo ya Kiserikali
ya Ikupa Trust Fund, Peter Charles, kwa ajili ya kusaidia miradi ya
akina mama na watoto wenye ulemavu nchini baada ya kuongea na waandishi
wa habari.
Baadhi
ya viongozi wa vijiji vinavyo zunguka mgodi wa North Mara, wakisiliza
hotuba ya Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow (hayupo
pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uwekezaji wa
kampuni na mchango wake katika kukuza uchumi wa kijamii wa Tanzania.
Kampuni
ya Barrick Gold Corporation (NYSE: GOLD) (TSX:ABX) – Imetambulika kama
mchangiaji mkubwa wa mapato ya Serikali katika mwaka 2021, na hivyo
basi, kuthibitisha nafasi yake kama mchangiaji mkubwa katika ukuzaji wa
uchumi wa kijamii Tanzania.
Rais
na Afisa Mtendaji Mkuu Mark Bristow, ameviambia vyombo vya habari hapa
leo kuwa tangu kampuni ianze kuendesha migodi ya North Mara na
Bulyanhulu mnamo mwezi Septemba 2019, jumla ya uwekezaji wake ni thamani
ya Dola bilioni $1.995 za Kimarekani1. Katika nusu ya kwanza ya mwaka
huu, imelipa dola milioni $158 za Kimarekani kama kodi, mirabaha na
ushuru; gawio kwa Serikali pamoja na mikopo ya uwekezaji yenye thamani
ya dola milioni 42 za Kimarekani; na dola milioni 210 za Kimarekani kwa
wazabuni wa ndani. Hadi hivi sasa, kampuni ya Barrick imekwishalipa dola
milioni $140 kati ya dola milioni $300 za Kimarekani za maafikiano na
Serikali.
“Tulipoingia
ubia na serikali na kuanza kuiendesha migodi hii, ilikuwa ni mzigo
mzito kwa Serikali na wawekezaji wao. Katika kipindi cha muda mfupi
tulifanikiwa kuisuka upya, na kutengeneza kile ambacho kimsingi ni
migodi miwili mipya. Migodi hiyo, hivi sasa, ipo katika nafasi nzuri ya
kufikia uzalishaji wa kila mwaka unaotokana na miongozo iliyopewa na
kampuni. Aidha, hivi sasa migodi ya North Mara na Bulyanhulu kwa pamoja
inayo uwezo wa kufikia ngazi ya hadhi ya pamoja ya daraja la kwanza la
uzalishaji (Tier 12 Complex). Hali hii ina inamaanisha kwamba migodi hii
miwili kwa pamoja, inayo uwezo wa kufikia uzalishaji wa wakia angalau
500,000 za dhahabu kwa gharama zilizo chini ya wastani wa sekta ya
uzalishaji wa dhahabu kwa kipindi cha zaidi ya miaka,” alisema Bristow.
"Tunaendelea
kuchukua hatua endelevu kwenye maeneo tunayochimba madini na kuhifadhi
mazingira katika migodi yote miwili na tunalenga fursa mpya pia. Katika
hili, tumeendelea kujiimarisha katika maeneo ya Bulyanhulu kutokana na
kupata leseni sita za kutafiti madini katika maeneo yanayopakana Jirani
na mgodi huo. Aidha, tumewekeza katika kuboresha mifano (models) ya
kijiolojia katika eneo la Kaskazini mwa Mkoa wa Mara na kubaini fursa
katika sehemu nyinginezo za uwekezaji nchini Tanzania.”
Hali
kadhalika katika kuhakikisha wazawa wanapewa kipaumbele shughuli za
kampuni hiyo, na kwa mujibu wa sera ya Barrick ya ajira za ndani, wazawa
wa Tanzania sasa wanachangia asilimia 96% ya nguvu kazi katika migodi
yake miwili. Aidha, asilimia 64% ya wasimamizi wao wakuu wakiwa ni
Watanzania. Migodi hiyo pia inayo dhamira ya dhati ya kuongeza ajira za
Wanawake katika tasnia ya uchimbaji madini ambayo kwa muda mrefu imekuwa
inaendeshwa na Wanaume kupitia mipango madhubuti inayolenga kuwaajiri
na kuwaendeleza wafanyakazi hao.
Katika
uwajibikaji kwa jamii, Barrick imetenga Dola 6 za Kimarekani kwa kila
wakia moja ya dhahabu inayouzwa na migodi hiyo miwili kwa ajili ya
kuboresha huduma za afya, elimu, miundombinu na upatikanaji wa maji safi
ya kunywa katika jamii zinazoizunguka migodi hiyo.
Dola
nyingine milioni 70 za Kimarekani zimetengwa kwa ajili ya uwekezaji
katika miradi ya kitaifa ya inayolenga kuongeza thamani kwenye miradi
mbalimbali ya kitaifa, inayojumuisha mafunzo yanayohusu madini na vifaa
vya kisayansi katika vyuo vikuu vya Tanzania.
Katika
nyanja ya usalama kazini, mgodi wa Bulyanhulu ulitangazwa kuwa mshindi
wa jumla wa tuzo ya Tanzania ya OSHA (Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali
pa Kazi) kwa mwaka 2022 huku ule wa North Mara ukitunukiwa tuzo ya
mpango bora wa uhamasishaji wa afya ya jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...