Mhifadhi katika Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi Waida Salmin Masambuli(kushoto) akielezea jambo kwa baadhi ya wageni kabla ya kuanza kutembelea vivutio vilivyopo ndani ya msitu huo.
Na Said Mwishehe ,Michuzi TV
KATIKA msimu huu wa Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) wameamua kutoa ofa kwa Watanzania kutembelea hifadhi ya Msitu wa mazingira asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
TFS iliweka wazi pamoja na kuwa na banda lao katika Maonesho hayo lakini wameweka mpango maalumu kupitia ofa ya Sabasaba wananchi kupata nafasi ya kutembelea msitu wa Pugu Kazimzumbwi kushuhudia utajiri wa vivutio vya utalii vilivyomo ambapo mtalii akiingia atatamani kurudi mara kwa mara.
Kutokana na ofa hiyo Julai 10,2022 wananchi kutoka maeneo mbalimbali wamepata nafasi ya kutembelea msitu huo kwa ajili ya kuona vivutio vya utalii na wengi wamevutiwa na kutoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii vya TFS.
Akizungumza na Michuzi TV pamoja na Michuzi Lissa Makesy ambaye ni miongoni mwa walifika kwenye msitu huo kutokana nan a ofay a TFS katika msimu huu wa Sabasaba amesema amevutiwa na vivutio vya utalii ambavyo ameshuhudia katika msitu huo likiwemo bwawa kubwa lenye samaki, mti wa Mpugupugu, ndege , misitu ya asili na kubwa zaidi ni pale eneo ambalo jijini la Dar es Salaam linaonekana lote kama lilivyo.
“Binafsi natoa shukrani zangu kwa TFS kwa kuamua kutoa ofa hii ya sisi wananchi kuja kutembelea msitu huu, kuna vivutio vingi ambavyo sikuwahi kufikiria kama vipo katika eneo hili lakini sasa nitakuwa balozi kwa kuhamasisha wengine waje waone.Ni kuzuri sana na ukifika hapa utafurahia mazingira jinsi yalivyo,”amesema Makesy.
Wakati huo huo Salama Jumbe Salehe ambaye naye amefanya utalii kwa kutembelea msitu huo amewapongeza TFS kwa kuandaa safari ya watu kwenda katika msitu huo kujionea utalii uliomo na yeye mbali ya kuona ndege na mitu mingi amevutiwa na milima iliyopo ndani ya msitu huo ambayo inakupeleka eneo ambalo unaliona Jiji la Dar es Salaam.
“Tumeona ndede wengi, tumeona miti mingi mizuri, tumeona misitu mizuri, hivyo tuendelee kutembelea maeneo yetu ya vivituo vya utalii.TFS wamefanya kitu kizuri kuandaa siku kama ya leo kutuletea hapa,”amesema.
Kwa upande wake Mhifadhi katika Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi Waida Salmin Masambuli amesema wametembelewa na wageni hao ambao wametokana na ofa ya Sabasaba waliyoiandaa kwa ajili ya kutangaza vivuti vyao vinavyopatikana na waliona wasiishie tusiishie tu kutangaza pale pale Sabasaba.
“Hivyo tuliona twende mbele zaidi kwa kuandaa ofa ya chini kabisa ambayo wageni(Watalii) wanaweza kuimudu na na kuja kuona uhalisia.Tunashukuru muamko wa kuja kutembelea hifadhi hii umekuwa mkubwa na wageni kutembelea mahali hapa. Wameona vivutio vyetu na wamefurahia,”amesema.
Ametoa rai kwa watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii kwani hawataboreka bali watapenda na kufurahia.“Tunawakaribisha Watanzaia wote mje kwenye msitu wetu wa mazingira asilia Pugu Kazimzumbwi.”
Matukio mbalimbali katika picha baada ya baadhi ya wananchi kutembelea Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi.Wananchi hao ambao ni watalii wa ndani wamefika kwenye Msitu huo kutokana na ofa ya msimu wa Sabasaba iliyotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS.)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...