Benki ya NMB imeendelea kujidhatiti kibiashara na kujiimarisha kulihudumia taifa kupitia mtandao wake wa matawi ambao sasa umefikia matawi 227 kufuatia uzinduzi wa tawi la NMB Buhongwa mkoani Mwanza.
Akizungumza kabla ya ufunguzi rasmi wa tawi hi hilo Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Bw. Filbert Mponzi, alisema kati ya mwaka 2019 na 2021, NMB iliisaidia serikai kukusanya mapato yenye thamani ya TZS trilioni 8.6.
Akifafanua mchango wa NMB katika juhudi za maendeleo za serikali, Bw. Mponzi alisema sasa hivi Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) una zaidi ya taasisi 1,100 zilizounga mifumo yake kwenye mifumo ya NMB ya ukusanyaji wa mapato.
Aidha alisema kuwa pamoja na mtandao mpana wa matawi, pia NMB imeendelea kutumia tekinolojia kufikisha huduma zake kwa watanzania wengi zaidi na kulihudumia taifa kwa ujumla.
Bw. Mponzi alisema tawi hilo jipya ambalo ni la 13 mkoani Mwanza na 38 Kanda ya Ziwa, ni tawi kamili lenye huduma zote za kibenki, zikiwemo zile za mikopo kama kuwakopesha wakulima.
NMB imekuwa mstari wa mbele katika jitahada za serikali za kuimarisha kilimo nchini na tayari imetoa mikopo ya kilimo ya TZS bilioni 100 kwa riba nafuu.
Tawi hili la NMB Buhongwa ni tawi kamili lenye huduma zote za kibenki yaani huduma za miamala, mikopo, ushauri, kufungua akaunti, kufanya huduma za kubadiri fedha za kigeni, huduma za bima na hata ushauri wa masuala ya biashara na fedha,” Bw Mponzi alinena na kuongeza:
Kwa upande wake Mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo ya uzinduzi Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Sauda Msemo, alisema kuwa, NMB Pamoja na kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi hadi vijijini kupitia matawi, vituo vya huduma na mawakala, ni mshiriki na mdau muhimu katika juhudi za Serikali za kuboresha huduma za kijamii kwa kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbaili hasa za elimu na afya.
Naibu Gavana huyo pia aliipongeza NMB kwa kutenga zaidi ya 200 bilioni kwa ajili ya mikopo yenye riba nafuu kwenye sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Sauda Msemo (wa pili kushoto) akikata
utepe ili kuzindua tawi la NMB Buhongwa jijini Mwanza, wa katikati ni
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi, Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi(kushoto), Meya wa jiji la Mwanza
Sima Costantine (wa pili kulia) na Meneja wa NMB kanda ya Ziwa – Baraka
Ladslaus wakishuhudia.
Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Sauda Msemo (wa tatu kushoto) akikata
utepe ili kuzindua tawi la NMB Buhongwa jijini Mwanza juzi, wanne
kushoto ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert
Mponzi, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi(wa Pili kushoto),
Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula (kushoto),Meya wa jiji la Mwanza
Sima Costantine (wa pili kulia) na Meneja wa NMB kanda ya Ziwa – Baraka
Ladslaus wakishuhudia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...