Chama Cha Mapinduzi  kimeipongeza serikali  kwa kazi kubwa ya kuboresha sekta ya afya nchini kwa vile inagusa maisha na ustawi  wa Taifa.

Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka ametoa pongezi hizo leo baada ya kufanya ziara ya kutembelea  hospitali ya taifa ya Muhimbili pamoja na taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kutathmini utendaji na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM.

‘’Tumejionea mabadiliko makubwa sana katika sekta ya afya..kwa kweli tulikotoka ni tofauti na hapa tulipo.hapa tulipo ni bora sana Mapinduzi na mageuzi makubwa  katika sekta ya afya tunayoyasikia nje na uhalisia ukifika hapa ni tofauti sana kazi kubwa sana imefanyika’’ alisema Shaka.

Amefahamisha kuwa dhamira na utayari wa Rais Samia Suluhu Hassan kutenga fedha katika budjeti ya serikali  shilingi bilioni 630 kwa ajili ya ujenzi  wa hospitali hiyo ya Muhimbili inakwenda kuandika historia mpya katika nchi ikizingatiwa hospitali hiyo imekuwa ni kimbilio ndani na nchi za jirani.

‘’Hospitali hii imejengwa mwaka 1905 wakati huo ikihudumia watu 1,100 kwa mwaka na hivi sasa imekuwa ikihudumia wagonjwa 3000 kwa siku lakini miundo mbinu ni chakavu hasa majengo ambayo mengine yamedumu kwa zaidi ya miaka 70 maono ya Rais Samia ni ukombozi mpya katika Sekta afya nchini ’ alisema Shaka

Amebainisha kuwa uwekezaji mkubwa katika hospitali ya Muhimbili ni kielelezo cha mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya CCM ibara 83  (p)  ambapo leo hii huduma za kibingwa na ubobezi zimekuwa zikitolewa nchi na sio nje ya nchi kama ulivyokuwa imezoeleka na kupelekea kupunguza kwa kiasi kikubwa rufaa za nje ya nchi na kupunguza mzigo kwa serikali katika kulipia gharama za matibabu.

Katika hatua nyingine katibu itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka  pia alimtembelea na kumjuilia hali mama ambaye watoto wake walifanyiwa upasuaji wa kutenganishwa ambao waliungana.

‘’Tanzania kwa mara nyingine inaingia katika historia za utabibu bora na bingwa kufanyika katika nchi yetu,  katika eneo la Afrika mashariki kufanyika upasuaji huu ni mara ya kwanza na katika Afrika Tanzania inakuwa nchi ya tatu kufanya upasuaji mkubwa kama huu tukitanguliwa na Afrika Kusini na Misri hii inaonesha ni namna gani uwekezaji huu ambao umefanywa kwenye sekta ya afya umeanza kuzaa matunda..Tunampongeza Rais Samia na serikali kwa nia yake ya dhati katika kuboiresha sekta hii ya afya’’ alisema Shaka

Shaka alitembelea taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ambako alielezwa na Mkurugenzi wa taasisi hiyo Profesa Janabi jinsi taasisi hiyo ilivyokuwa mkombozi katika ukanda huu wa afrika mashariki na kati.

Amefafanua kuwa serikali ilikuwa ikitumia Zaidi ya dola za kimarekani millioni 1.6 kwa mwaka kwa ajili ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu kati ya 200 hadi 300, lakini toka kuanza kwa taasisi hiyo  imepunguza mzigo huo kwa serikali kwa kiasi cha asilimia 95.

‘Ndani ya kipindi cha miaka 3 tumeweza kutibu wagonjwa wa moyo 8, 600 ndani na nje,  Sasa hapa tujiulize ingechukua miaka mingapi wagonjwa hawa kupata matibabu kama wangekuwa wanapelekwa hakika ukombozi huu ni wakujivunia, niwahakikishie serikali ya CCM itaendelea kuwekeza katika upatikanaji wa vifaa tiba, kuwaendeleza kimasomo wataalamu wetu sambamba na kuendelea kuboresha mazingira bora ya kutolea huduma"   alisema Shaka wakati  akitembelea wagonjwa waliyolazwa katika wodi mbalimbali na katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo  alikutana na mgonjwa kutoka Rwanda ambaye amemleta mtoto kufanyiwa upasuaji wa moyo.
























Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...