Na. WAF - Dodoma

Wasimamizi wa taaluma ya Maabara wa Mikoa wametakiwa kwenda kusimamia utoaji wa huduma bora na kufanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wengine kwa lengo la kuboresha huduma za Afya kwa wagonjwa.

Hayo yamesemwa na  Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza Dkt. James Kiologwe kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe kwenye mafunzo elekezi ya wasimamizi wa taaluma ya maabara wa mikoa jijini Dodoma.

"Mambo ambayo nimetumwa kuja kuwaeleza ni pamoja na kutambua kuwa mmechaguliwa kati ya wengi lakini mmeaminiwa, kipaumbele cha Serikali ni ubora wa huduma". Amesema Dkt. Kiologwe

Ubora wa huduma unaambatana na wataalamu wenye maadili ya kitaaluma na wenye kutoa huduma bora na kufanya kazi kama timu (Team work).

"Nendeni mkajipime kama mnaona hamtoshi kweye hiyo nafasi mliyochaguliwa basi rudini kwa wasajili muwaeleze kuwa mimi hapa siwezi, kazi hii ni kubwa kwangu, ili akae mtu anayefaa lakini naamini hapa wote mliochaguliwa mnafiti". Amesema Dkt. Kiologwe

Pia, wataalamu hao wametakiwa kwenda kuhakikisha kuwa wale ambao hawajasajiliwa wanasajiliwa ili kuendelea kuboresha huduma za Afya pamoja na kudhibiti mapato ya Serikali.

Naye, Msajili wa Wataalamu wa Maabara nchini Bi.Mary Mtui mafunzo hayo yatawapa uwezo wasimamizi hao uwezo wa kujua namna ya usimamizi shirikishi kwa kuwa wanaenda kusaidia kuimarisha na kusimamia eneo hilo pamoja na kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu,kanuni na sheria zilizopo kwa kufuata miiko na maadili ya taaluma ya Maabara nchini

Mafunzo hayo yanayofanyika kwa  siku mbili yana  lengo la kupeana maarifa zaidi juu ya uelewa wa sheria, kanuni na taratibu za namna ya kuongoza na kusimamia maabara ili kuongeza ubora na ufanisi katika kuwahudumia wagonjwa.

Katika mafunzo hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi msaidizi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka wizara ya Afya, Mkurugenzi idara ya Afya OR - TAMISEMI na wengine kutoka wizara ya Afya akiwemo msajili baraza la wataalamu wa maabara, msajili bodi ya maabara binafsi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...