
Kutoka Kushoto Meneja Mradi wa Kituo Cha Kupozea Umeme Chalinze kutoka Kampuni ya Shaker Consultancy Group Wael Nashat Aziz katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge na Meneja Msaidizi wa Mradi huo kutoka Kampuni ya TBEA AmyJiang wakifafanua jambo kwenye eneo hilo ambalo unejenzi unaendelea.
Na Khadija Kalili, Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge (RC), amesema kuwa changamoto ya umeme ndani ya Mkoani Pwanj inakwenda kubaki historia hiyo ni baada ya kufanya ziara ya kikazi katika vituo vitatu vya kupoza nishati ya Umeme ambavyo ni Chalinze , Mlandizi na Luguruni kilichopo maeneo ya Mloganzila.
RC amesema kuwa uwekezaji wa Kituo Cha Kupozea Umeme Cha Chalinze kimegharimu zaidi ya Bil.130 hivyo Kituo hicho kutakua ni kikubwa nchi nzima.
"Pwani ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni nyingine na ndani ya muda mfupi inakwenda kuchukua nafasi ingine ya kiuchumi ndani ya nchi hii" alisema RC Kunenge.
Kutokana na uwekezaji huu mkubwa ndani ya Mkoa wa Pwani hasa kwenye sekta muhimu ya nishati ya umeme natumia fursa hii kuwaita wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza huku lengo kuu ni kukuza uchumi wa nchi yetu kwa ujumla"alisema RC Kunenge.
"Pwani tunawakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ili waweze kuja kuwekeza kwa kujenga viwanda vikubwa kwa sababu kuna umeme wa uhakika pamona na maeneo ya kutosha"alisema RC Kunenge.
" Serikali imewekeza kwa kiwango cha juu sana tuna uhakika utapatikana umeme mwingi na wa uhakika na zile changamoto zote ambazo wawekezaji wetu walikua wakizipitia zitabaki kuwa historia" amesema.
"Serikali ina imani kubwa kwamba jinsi hali ilivyo viwanda vitaongezeka kwa wingi, ni kweli tulikua na changamoto ya umeme hivyo Kituo hiki cha Luguruni ambacho kimeanza kutoa huduma mwezi mmoja uliopita kimesaidia kupunguza changamoto ya umeme Pwani" amesema.
Mhandisi Mahawa Cosmas Mkaka ambaye ni Meneja wa Shirika la Umeme Wa Pwani (TANESCO) amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa kufanya ziara kwenye vituo vitatu vya uzalishaji wa umeme huku akisema kuwa Kituo Cha Luguruni kinalisha umeme katika meneo ya Kiluvya, Mailimoja, Lulanzi, Pangani,Picha ya Ndege na Kwa Matias na Kongowe pamoja na kiwanda cha TAMCO.
"Kwa namna ya kipekee namshkuru RC Kwa kutembelea vituo vyetu vya kupoza umeme ambapo ameweza kutembelea na kuona hali halisi ya vituo vyetu alisema Injinia Mahawa.
Amepongeza kwa kusema kuwa milango iko wazi kwa wateja wao kuweza kuwaandikia endapo kutatokea changamoto ya aina yoyote ya upatikanaji wa nishati ya hiyo ya umeme.
Akizungumza kuhusu namna walivyoimarisha miundombinu ya umeme kupeleka Kituo cha TAMCO, amesema kuwa hivi sasa watakua wakipokea umeme kutoka Luguruni huku urefu wa namna ya upatikanaji wa umeme ukiwa umemalizika kwa sababu hivi sasa umbali umepungua kwani hivi sasa umbali ni Kilometa 10 tofauti na ilivyokua zamani umbali ulikua ni KM.24 ambapo walikua wakichukua umeme kutoka Kituo Cha Mlandizi.
Meneja wa Kituo Cha Chalinze amesema kuwa Kituo Cha Chalinze kitakamilika mapema mwakani huku akifafanua kuwa kinapokea umeme kutoka katika bwawa la Mwalimu Nyerere hivyo Wilaya ya Bagamoyo nayo itanufaika kwa sababu watajenga Kituo Cha Zinga,pia kutajengwa line ingine itakayokwenda Mkuranga Rufiji, Kibiti Katika Kituo hiki tutanufaika sana Kwa sababu maeneo ya Mlandizi, Chalinze na Kibaha laini nyingine itakwenda hadi kwenye Kituo cha Kinyerezi.
Naye Meneja Mradi wa Kituo Cha Luguruni Mhandisi Dickson Lucian alisema Kituo cha Luguruni kimekamilika na tayari kimeanza kutoa huduma japo bado mambo kuna mambo madogomadogo hayajakamilika huku akitaja maeneo yanayopokea umeme kutoka kwenye kituo hicho kuwa ni Kiluvya, Mailimoja Lulanzi,Pangani,Picha ya Ndege, Kwa Matias, Kongowe pamoja na TAMCO.

Mitambo ya kupooza umeme.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...