Na Mwandishi Wetu, Rufiji

MKUU wa Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani Meja Edward Gowele amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya filamu ya Royal Tour ambayo kwa ujumla  Wilaya hiyo imepokea wageni wengi  na hivyo  wanakwenda kuongeza uchumi.

Aidha amewapongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) ambao wameandaa tour ya ofa ya msimu wa Sabasaba kwa vijana wa Kitanzania wakiwemo wanachuo na ambao sio wanachuo kutembelea vivutio ambavyo vipo wilayani Rufiji.

"Wageni wetu hao ambao wameletwa TFS  Kutokana na ofa ya Sabasaba wakiwa hapa Rufiji wamebahatika kuona vivutio mbalimbali,mfano chemchem ya maji moto,pia wametembelea jengo letu la kiutawala la Mkuu wa Wilaya, lakini   wametembelea maeneo ya mto wa Rufiji na kupata mandhari nzima ya Rufiji,kwa hiyo niwapongeze kwa hicho walichokifanya,", amesema.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Rufiji amesema wanamini kwa kufanya utalii huo wameunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuitangaaza nchi au kuvutia utalii ndani ya nchi lakini pia wamesapoti kazi kubwa ambayo Rais ameifanya ,kwa hiyo amewapongeza TFS Kwa kazi wanayoifanya.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...