Na Ripota Wetu,Ngorongoro

DIWANI wa Kata ya Kakesio iliyoko Tarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha amesema ameamua kwa hiyari yake kuhama katika hifadhi ya Ngorongoro na kwenda Msomera wilayani Handeni kwa lengo la kuwa na hatma njema ya yeye na familia yake.

Akizungumza leo Julai 7,2022 alipokuwa akitangaza uamuzi wa kuhama kwa hiari mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Balozi Pindi Chana pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali na wananchi ,Diwani wa kata ya Kakesio Johaness Tiamasi amesema siku ya leo ataihesabu kama siku ya historia katika maisha yake.

“ Mimi kama diwani wa kata ya Kakesio na nafasi nyingine ambazo nimeshika, mimi katika halmashauri yetu ni Mwenyekiti wa Kamati ya huduma za kijamii kwa maana ya elimu, afya na maendeleo ya kijamii. Mimi ni kiongozi wa jamii.

“Nimeanza kuongoza tangu mwaka 1993 kwa kufanya kazi ya mtendaji kwa miaka saba na ndio watendaji wa kwanza,nimekuwa Mwenyekiti wa kijiji kwa miaka 10,nimekuwa diwani kwa miaka 15 na ninaendelea na nafasi hiyo hadi sasa.

“La muhimu kwangu nimesema la historia kwa sababu nimeamua kwa hiari yangu na kwa akili zangu timamu kwamba ni wakati wa sasa kwa karne kubadilisha makazi,nimekaa huku sana na ni mwenyeji, tangu babu yangu,baba yangu na wazazi wangu akiwemo mama wote wamezikwa kule,” amesema.

Ameongeza licha ya kuwa ya kukaa Ngorongoro kwa muda mrefu lakini haoni kesho ya watoto wake, hivyo ameona afikirie mbali kwasababu ni vema akawa na maono ya mbali kuliko kufikiria karibu,.” Tanzania ni moja, nchi yetu ni moja na Mungu ni mmoja nikasema mimi kwa hiari yangu.

“Namuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwasababu ametengeneza maono ya baadae ya watoto hawa wa kifugaji ambao wamekaa pale miaka yote hawakuwa wanafanya jambo lolote ambalo linawabadilisha au linaweza kubadilisha mitazamo ya maisha yao.

“Dunia hii huwezi kubaki na kitu kimoja, lazima
Ulime, lazima ufanye kitu zaidi ya kimoja inaweza kuwa kitega uchumi ambacho kitakusaidia wewe na familia yako , kwa hiyo nikasema nimuunge Rais mkono,nikasema ninahamia Msomera wilayani handeni mkoani ili nikaungane na watanzania wenzangu, wana Ngorongoro wenzangu ili tukaanze maisha mapya kule.”

Amesema amefanya hivyo na ameungwa na kaya yake na mara ya kwanza alipoenda kwa Mkuu wa Mkoa alienda na kaya 29 na tayari yuko na kaya 11 na nyingine zishafanyiwa tathimini na watamfuata kupitia utaratibu utakaowekwa.

“Nitoe shukrani zangu kwa mkuu wa wilaya yangu nilipoomba ushauri walinishauri vizuri. Mkuu wa mkoa ulinishauri vizuri na nimekubaliana na ushauri huo kwasababu najua niko sehemu salama ,nawashukuruni sana,pia niwashukuru wana mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro nimefanya kazi nao miaka mingi kweli, yaani mimi nimefanya kazi na wahifadhi wengi sana na mpaka leo Dk.Manongi.

“Tumefanya kazi pamoja na licha ya changamoto za uhifadhi bado tumeendelea kuheshimiana na hatujukwaruzana , nawashukuru wote na tutaendelea kuwa wamoja.Katiba yetu inatupa uhuru wa kuishi kokote pale ilimradi usivunje sheria kwa hiyo ni uhuru wa madiwani wenzangu ambao niko nao sitawaacha tutawasiliana ,tutaongea na wengine kwamba ni vizuri tukatii mamlaka za nchi kwasababu hata biblia inatuambia mamlaka ziliopo zinatoka kwa Mungu,amesema diwani huyo

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana akiagana na Diwani wa kata ya Kakesio Johaness Tiamas ambaye ameamua kuhamia Msomera kwa hiari yake kupisha shughuli za uhifadhi katika eneo la Ngorongoro,ambapo Waziri Pindi Chana aliziaga kaya 36 zinazohama kwa hiari kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera kilichopo Wilaya ya Handeni mkoani Tanga kwenye hafla fupi leo katika Ofisi za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro zilizopo wilayani Karatu mkoani Arusha.Pichani kati ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Raymond Mwangala akishuhudia.PICHA NA MICHUZI JR-NGORONGORO.

Diwani wa kata ya Kakesio Johaness Tiamas ambaye meamua kuhamia Msomera kwa hiari yake kupisha shughuli za uhifadhi katika eneo la Ngorongoro akizungumza mbele ya Waziri Pindi Chana,Viongozi wengine mbalimbali wakiwemo wakaazi waliokuwa wakiishi eneo la Ngorongoro ambao nao walikuwa wakiagwa rasmi kuelekea Msomera,Handeni mkoani Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongera akipeana mkono wa kwaheri na Diwani wa kata ya Kakesio Johaness Tiamas ambaye meamua kuhamia Msomera kwa hiari yake kupisha shughuli za uhifadhi katika eneo la Ngorongoro,Pichani kati ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana akishuhudia

Naibu Kamishna wa NCAA huduma za Shirika Needpeace Wambuya akipeana mkono wa kuagana na Diwani wa kata ya Kakesio Johaness Tiamas ambaye meamua kuhamia Msomera kwa hiari yake kupisha shughuli za uhifadhi katika eneo la Ngorongoro,Pichani kati ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana akishuhudia


Pichani ni baadhi ya waliokuwa wakaazi katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro wanaohamia Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga kwa hiari kupisha shughuli za uhifadhi wakimsikiliza kwa makini maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana alipokuwa akiwaaga rasmi leo.

PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-NGORONGORO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...