WANANCHI wa kaya 104 waliohamia Kijiji cha Msomera wilayani Handeni wakitokea Hifadhi ya Ngorongoro wamepatiwa vyandarua vitatu kwa kila nyumba sambamba na elimu sahihi ya matumizi ya chandarua ili kujikinga na malaria pamoja na magonjwa mengine yanayotokana na mabaadiliko ya hali ya hewa.
Akizungumza wakati wa kugawa vyandarua hivyo kwa wananchi hao walioamua kuhama kwa hiari yao kwenye hifadhi hiyo na kuhamia Kijiji cha Msomera ,Tabibu Mwandamizi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Grace Vincent amesema eneo la afya ni muhimu , hivyo wameamua kugawa neti hizo kwa wenzao waliotoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro waliohama kwa hiari yao wenyewe.
“Eneo la afya huwa tunajali sana afya za wakazi hao na hivyo tumenunua vyandarua kujikinga na mbu. Kwasababu Wilaya ya Handeni ni Wilaya mojawapo yenye maralia nyingi , sasa na wao wametoka maeneo yenye muinuko wa juu ambako mbu huwa hawakai.
“Kutokana na hali hiyo tutakuwa nao sambamba na wananchi kwa kuhakikisha wanapata elimu ya vyandarua na tutaitoa nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha wanaenda kuzifunga ndani ya usimamizi na tunahakikisha wanakuwa ndani ya neti hizo ili wasipate malaria kwani kubadilisha hali ya hewa inaweza kuathiri afya zao na sasa tunasema kinga ni bora kuliko tiba.”
Tabibu huyo ameongeza na sio kutumia chandarua tu bali kutumia kwa usahihi maana unaweza kuweka kichwani na ukaacha kufunika miguu wakati miguu nayo ni sehemu ya mwili ambao unaweza kung’atwa na mbu.Unaweza ukawa hujaweka vizuri chandarua , hivyo mbu naye anapata nafasi, hivyo unatakiwa kuhakikisha unaweka neti vizuri ili mbu asipate nafasi,”amesema.
Amefafanua kuwa utaratibu wao wanagawa vyandarua vitatu kwa kila nyumba na wanatoa idadi hiyo kwasababu kila nyumba inavyumba vitatu na lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha wenyeji wao waliotoka Hifadhi ya Ngorongoro wanapata kinga au wanapata tahadhari , kule Ngongoro walikotoka hakuna majani, maana yake mazingira ya kule yako kwenye maeneo ya muinuko hivyo mbu hawezi kuishi vizuri lakini unapobadilisha hali ya hewa ni lazima tuhakikishe unapata huduma nzuri za afya ili miili yao iimarike ili wasije kupata maradhi yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa.
Aidha amesema iwapo kuna mtu anatumia dawa zake kwa muda mrefu wakifika wataungana na wenzao ili kuhakikisha anaendelea kupata wakati kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kupata chanjo kwa usahihi na kwa mama mjamzito watahakikisha anaendelea kwenda kliniki yake ili kujifungua salama.
“Kwa hiyo sisi idara yetu ya afya na kitengo chetu cha zana cha Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro itahakikisha kwanza ni afya ambayo iko sahihi na kwamba wanashauri uangaliaji afya za wakazi hao unatakiwa kufanyika kwa miezi sita.
Kwa upande wake Masiaya Laizer ambaye ni miongoni mwa wakazi walionufaika na elimu hiyo ameishukuru Serikali kupitia NCAA kwa kutuma wataalam wake kuwapa elimu hiyo na kuongeza uelewa wa namna wa kujilinda na kujikinga dhidi ya maambukizi ya malaria katika mazingira hayo mapya.
“Mimi nilitoka Kijiji cha Esere Ngorongoro, kule ni mazingira ya baridi na hakuna mbu. Msomera ni mazingira tofauti na baridi ni ya kawaida na wakati mwingine joto hivyo elimu hii ni muhimu sana kwetu ili tujikinge pamoja na Watoto wetu” aliongeza Laizer.”
Tabibu Mwandamizi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Grace Vicent akeieleza jambo wakati akitoa elimu kwa WANANCHI wa kaya 104 waliohamia Kijiji cha Msomera wilayani Handeni wakitokea Hifadhi ya Ngorongoro namna ya kutumia vyandarua kwa usahihi ili kujikinga na malaria pamoja na magonjwa mengine yanayotokanayo na mabaadiliko ya hali ya hewa.Chini ni picha mbalimbali zikionesha namna gani ya kutumia vyndarua hivyo kutoka kwa Wataalamu wa NCAA.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MSOMERA-HANDENI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...