Waziri wa Nishati na Madini January Makamba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara katika mikoa 14 kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake, jijini Dar es Salaam.



*Adai kero zote zitatolewa ufumbuzi  katika kuhakikisha wananchi wanasikilizwa hasa wa vijijini

Na Chalila Kibuda,  Michuzi TV

 WAZIRI wa Nishati Januari Makamba kwenda siku 21 katika mikoa 14 na Wilaya 38 kwenye mikoa hiyo kwa kukagua miradi inayotekelezwa na Wizara na Taasisi za  Wizara hiyo.

Ziara katika mikoa hiyo Waziri Makamba atafanya mazungumzo na wananchi kwa kupokea kero zao sambamba na maoni, ushauri   katika mambo yote hayo atatoa majibu na ufumbuzi kwenye sekta ya nishati pamoja na kwenda na vipaumbele vya Wizara kwa mwaka wa ujao wa fedha.

Makamba ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Julai 10 , 2022 kuhusiana na ziara hiyo anayotarajia kuanza Julai 11 itayohusisha Mikoa ya Mara, Mwanza, Geita , Simiyu, Kagera , Shinyanga, Tabora, Katavi Rukwa, Songwe, Mbeya , Ruvuma pamoja na Mtwara huku mikoa mingine iliyobaki itahusisha katika awamu zifuatazo zitazofanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Makamba amesema katika ziara hiyo maeneo yatakayopewa kipaumbele ni upatikanaji wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia, Uzambazaji wa umeme Vijijini na Vitongojini , Upatikanaji wa umeme wa uhakika, Uboreshaji wa huduma zitolewazo na taasisi na Wizara, Usambazaji wa mafuta salama na bei nafuu vijijini

Amesema lengo katika ziara hiyo ni kusogeza huduma za Wizara na Taasisi kwa wananchi hasa wa vijijini na pia kuongeza uelewa kwa watanzania kuhusu sekta ya nishati na mageuzi tunayoyafanya.
Aidha amesema inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itahakikisha kwamba sekta ya nishati itachangia katika ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania.

Waziri wa Makamba amesema kuhusiana na matumizi ya nishati ya kupikia wanannchi 22 wanafariki kutokana na matumizi ya kutumia nishati ya kupikia isiyo salama.

Hata hivyo kwa upande wa vijijini upande wa mafuta katika vyombo vya moto wanatumia mafuta yasiyo salama kutokana na uhifadhi na kusababisha kuu magari pamoja na pikipiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...