Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji(UWURA) imesema uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kutoa Sh.bilioni 100 kwa ajili ya kupunguza bei ya mafuta ni uamuzi ambao umekwenda kuleta unafuu mkubwa kwa Watanzania.

Akizungumza katika Maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa Meneja Mawasiliano Titus Kaguo amesema kwenye maonesho hayo wengi wanauliza kama Serikali imetoa Sh.bilioni 100 katika kupunguza bei ya mafuta na hizo zimetolewa na Rais Samia Suluhu ili kukabiliana na kupanda kwa mafuta .

“Ninachotaka kusema kwa watanzania kwanza wamuombee sana Rais wetu, wamshukuru sana na waendelee kutoa ushirikiano kwasababu anawafanikisha kuwa na maisha haya…

“Kwasababu kama Sh.bilioni 100 zisingetolewa leo mafuta ya Petrol kwa Dar es Salaam lita moja ingekuwa Sh.3497 na hiyo ni sawa na lita moja Sh.3500, Dizeli ingekuwa Sh.3510 kwa lita moja.

“Lakini kwa Sh.bilioni 100 ambazo Rais Samia ametoa imepunguza bei ya mafuta, lita moja ya Petrol kutoka 3,497 hadi Sh.3,220, Dizeli kutoka Sh.3510 hadi Sh.3140 , hivyo utaona hilo punguza ni kubwa,Waziri wa Nishati Januari Makamba anatakiwa kusifiwa , kwa kutenda kazi hizi, Rais wetu anatakiwa kusifiwa kwa kutenda kazi na hata kwa kuamua kutoa Sh.bilioni 100.  

“Hizi fedha angeweza kuamua kujenga vituo vya afya, kujenga barabara au kufanya mambo mengine kwani kuna mengi ya kufanya nchini kwetu.Angeweza kusema watanzania wanunue mafuta kwa bei ya soko la dunia .

“Lakini amesema hapana watanzania wangu wasiumie kwa bei ya soko la dunia.Hivyo pamoja na hali iliyopo leo bado imefanikiwa na Sh.bilioni 100 za Rais ambazo zimefanya hata bei ya mafuta iwe kwenye hizi bei ambazo zipo sasa,”amefafanua Kaguo.

Ametoa mfano Mkoa wa Mtwara kama isingekuwepo Sh.bilioni 100 ya Rais Samia mafuta yalishafikia Sh.3600, kwa hiyo  Serikali imetenda jambo kubwa sana na wao kama UWURA wanatekeleza maelekezo wanayopewa.

Katika hatua nyingine amefafanua kuhusu uhusiano wa kupanda kwa mafuta kutokana na vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine ambapo ametoa sababu tatu zinazosababisha mafuta kupanda.

“Niseme kwenye mfumo wa mafuta ya Petroli kuna vitu ambavyo vinaitwa tetesi , yaani kunapokuwa tesisi ya kitu fulani kwenye mafuta inapandisha bei.
“Kwa hiyo ilipoanza fununu tu Urusi na Ukraine watapigana kwenye biashara ya mafuta tayari ilishatengeneza biashara.Kwa kuwa Urusi ya Ukraine watapigana matumizi ya mafuta kwa nchi kwanza yatakuwa makubwa,”amesema Kaguo.

Amesema sababu ya pili Urusi imewekewa vizingiti kwamba isiuze mafuta yake na yeye anatoa asilimia karibu 10 ya mafuta ya dunia nzima.

“Hiyo asilimia 10 ndio watu wanapigania katika maeneo ambayo yanatoka mafuta Urabuni na maeneo mengine , kwa hiyo ile asilimia inasababisha mafuta yapande .

“Sababu ya tatu Urusi amezuiwa kusafirisha kwa maana nyingine ni kwamba meli zinazosafirisha mafuta Mrusi anazo meli kama 250 ambazo zinasafirisha mafuta.Kutokana na vikwazo hivyo meli zote hazisafirishi mafuta,”amesema.

Kutokana na hali hiyo inabidi zipatikane meli nyingine 250 kuziba nafasi hiyo, kwa msingi huo gharama za usafirishaji nazo zimepanda na ndio maana bei ya mafuta imepanda kila mahali kuanzia katika soko la dunia hadi katika usafirishaji wake.

“Niseme ukweli Serikali yetu imejitahidi , katika maeneo ambayo imefanya kazi kubwa ni hili la kupungua Sh.300 au 400 ni hela nyingi sio ndogo.

“Kwa mfano Tanzania kwa siku tunatumia lita milioni 10 hivyo ukizidisha mara 300 au 400 ni shilingi ngapi kwa serikali imepungua, tusizungumze kama mtu mmoja ananunua mafuta bali twende kama nchi na kiasi hicho ambacho kinatumika kwa siku,”ameeleza Kaguo.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti waNishati na Maji (EWURA)Titus Kaguo(kulia) akimuelezea jambo Waziri wa Nishati Januari Makamba (kushoto) kuhusu jarida ambalo limetengezwa na Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuelezea mambo mbalimbali wanayoyafanya.Waziri Makamba ametembelea banda la UWURA leo ambalo lipo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam.Wengine katika picha hiyo ni maofisa wa mamlaka hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA)Titus Kaguo(kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati Januari Makamba(kushoto) baada ya kutembelea katika banda lao ambapo pamoja na mambo mengine amumuelezea namna ambavyo fedha Sh.bilioni 100 ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan zinavyosaidia katika kupunguza bei ya mafuta nchini.
Waziri wa Nishati Januari Makamba (katikati) akizungumza wakati alipotembelea banda la EWURA lililopo katika Maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam.
Maofisa wa EWURA(kushoto) wakiendelea kuzungumza na baadhi ya wateja waliofika kwenye banda lao kwa ajili ya kufahamu masuala mbalimbali yanayohusu udhibiti wa nishati na maji.
Mmoja ya wananchi akitoa maoni yake kwa maofisa wa EWURA baada ya kutembelea kwenye banda hilo katika maonesho ya 46 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea Dar es Salaam.
Sehemu ya wananchi wakiendelea kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali baada ya kutembelea banda la EWURA.
Matukio mbalimbali katika picha yakiendelea katika banda la EWURA wakati wa maonesho ya 46 ya biashara ya kimataifa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...