

MKURUGENZI Mkuu wa Ewura, Mhandisi Modestus Lumato
amekutana na kufanya kikao kazi na wahariri wa vyombo mbali mbali kutoka
Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) kujadiliana juu ya matumizi mbadala
ya gesi kwenye magari na hata majumbani hususani Vijijini ambako
wamekuwa wakitumia zaidi kuni na mkaaa.
Katika
majadiliano hayo yaliyofanyika leo Julai 16, 2022 katika ukumbi wa
Kisenga millennium Tower eneo la Kijitonyama Dar es Salaam pamoja na
mambo mengine, Lumato amepokea ushauri mbalimbali kutoka kwa wahariri
hao na kujibu maswali huku pia wamejadili kupanda kwa bei za mafuta.
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile (kushoto aliyesimama) akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Mwandamizi Huduma kwa wateja wa EWURA Kanda ya Mashariki Getrude Mbiling'i akifuatilia mkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...