Msajili wa Baraza la Famasi nchini Elizabeth Shekalage akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa wanafunzi wa Famasia Afrika  uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha pamoja ya wadhamini wa mkutano wa Wanafunzi Wafamasia Afrika uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Wafamasia wakiwa na Bendera ya Tanzania wakati mkutano wa uliofanyika jijini Dar es Salaam.

 

 *Wakati umefika wa kwenda na mabadiliko ya teknolojia  katika sekta ya dawa

Na Chalila Kibuda , Michuzi TV

 WANAFUNZI na wahitimu wa hivi karibuni wa kada ya Famasi Afrika wamekutana katika kujadili kada hiyo namna watavyosaidia kwenda na na teknolojia katika sekta ya dawa.


Akizungumza wakati kufungua Mkutano wa Wanafunzi na Wahitimu wa Kada ya Famasi (IPSF) Msajili wa Baraza la Famasi nchini Elizabeth Shekalage amesema vijana kuwa kada ya Famasi kwa vijana wanatakiwa kusimamiwa katika kuweza kufanya mabadiliko katika sekta ya dawa kwa kutumia teknolojia.

Mkutano huo umefadhiliwa na wadau mbalimbali ikiwemo Mradi wa HPSS unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi  kwa lengo la kukuza kada ya famasi kwa wanafunzi.

Amesema kuwa mkutano huo ni mara ya pili kufanyika Tanzania mara ya pili ambapo ni fursa ya vijana ambao ni wanafunzi kujadiliana katika sekta ya dawa namna ya kuweza kutumia teknolojia katika kufanya utafiti wa dawa.

Shekalage amesema kuwa vijana hawa ndio wanaweza kuwa sehemu wawekezaji katika uzalishaji sekta ya dawa hivyo mikutano inaweka pamoja na kubadilishana uzoefu wa nchi na nchi.

Aidha amesema kuwa katika katika kipindi kilichopita dunia ilipita katika ugonjwa wa UVIKO 19 ambapo kada ya famasi bado iko katika kuendelea kufanya tafiti.

Mwenyekiti wa  Wanafunzi wa Kada ya Famasia Afrika   Dk.Moussa Fofana  amesema kuwa kama vijana wanawajibu kuimarisha kada ya Famasia na kutoa mchango katika kufanya tafiti kwenye sekta ya dawa kwenda na teknolojia.

Fofana amesema kuwa mkutano huo ndio kiungo muhimu katika kuunganisha Wafamasia na kujadili masula mbalimbali na kutoa suluhisho.

Aidha amesema kuwa katika kipindi wanafunzi lazima kuendelea kufanya tafiti ambazo zitasaidia katika kutoa dawa za kutibu wananchi kwa kuendana na mifumo ya  teknolojia.

Mshauri Mwandamizi wa Mradi wa HPSS unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi  Fiona Chilunda  amesema wanafunzi waendelee kuwa wazalendo katika kada ya Famasi katika kuleta matokeo chanya.

Amesema kuwa wanafunzi waendelee kufanya tafiti na kupenda masomo ya sayansi na kuja kusaidia wananchi katika huduma kwenye sekta ya dawa.

Mshauri wa mradi wa HPSS Fiona Chilunda akizungumza kuhusiana na mkutano wanafunzi wa Wafamasia Afrika kuwa wazalendo na kupenda sayansi , jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa mkutano wa wanafunzi wa wafamasia Afrika.
Mwenyekiti wa Wanafunzi wa Wafamasia Afrika Dk.Moussa Fofana akizungumza kuhusiana na mikakati mbalimbali ya mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...