Na John Walter-Manyara
WANANCHI wametakiwa kuwa tayari na kujitokeza katika sensa ya watu na makazi inalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

Aidha amewataka wenye watoto wenye ulemavu wasiwafiche watoto hao ili nao wapate haki yao ya msingi ya kuhesabiwa na pindi serikali inapoleta mahitaji kwa ajili ya kundi hilo asiachwe yeyote.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Paulina Gekul (Naibu waziri wa utamaduni sanaa na Michezo) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Maisaka akiwa katika ziara yake siku ya kwanza yenye lengo la kuwapa mrejesho wananchi na kusikiliza kero zao.

Amesema wananchi wanatakiwa kuwa tayari kuhesabiwa ili kuweza kuiunga mkono Serikali katika mipango yake ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.

"Wakati utakapofika tujitokeze kuhesabiwa kwa kufanya hivyo tutakuwa tumejitendea haki sisi wenyewe kwakuwa hatutarukwa na maendeleo." Amesema.

Amesema watau wakihesabiwa na kujulikana idadi yao kwa usahihi itasaidia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa pia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...