Wananchi wakiendelea kupata elimu na huduma  kwa Maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika Viwanja vya Mwalimu JK Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 

Na Mawandishi Wetu, Dar es Salaam  

WANANCHI na Wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wamefurahishwa na uboreshwaji wa  huduma za Mfuko huo ambazo kwa sasa zinapatikana kwa njia ya kielekroniki.

Hayo wameyasema kwa nyakati tofauti katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.

Akizungumzia kuridhishwa kwa huduma hizo, Bw. Andrew Elias ambaye alifika katika banda la NHIF kwa lengo la kupata huduma ya elimu na kujiunga na huduma za Mfuko.

"Ukweli huu ni bunifu sana, nimeona ambavyo mmerahisisha mambo ambapo kwa sasa taarifa zote za uanachama zikiwemo gharama unazotumia hospitali,  huduma ulizopewa na namna kadi yako iluvyotumika unazipata kupitia NHIF App haya ni mafanikio makubwa," alisema Bw. Elias.

Naye Mkazi wa Kipawa Bi. Roida Msembu ambaye alifika kwa lengo usajili, alisema kuwa gharama zinazotozwa na Mfuko zimezingatia uhalisia wa vipato vya wananchi hivyo akauomba Mfuko kufika katika maeneo mengi zaidi.

Akizungumzia ushiriki wa Mfuko katika Maonesho hayo, Meneja Uhusiano wa NHIF, Bi. Anjela Mziray alisema kuwa, Mfuko umejipanga kurahisisha zaidi huduma kupitia mitandao kutoa huduma bora na za haraka kwa wananchi lakini pia kuhamasisha wajiunge na huduma ili wawe na uhakika wa matibabu wakati wowote.

"Nawakaribisha wote wanachama na wasio wanachama kutembea banda letu la NHIF ambalo liko karibu kabisa na mlango Mkuu wa kuingilia ndani ya viwanja vya maonesho, NHIF tupo tayari kuwapa huduma ya elimu, kuwasajili na kutatua changamoto wanazokutana nazo katika kupata huduma," alisema Bi. Mziray.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...