Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja Yesaya Mwakifulefule wakati Mkuu wa Mkoa huyo alipotembelea Banda la Shirika la Taifa la Bima (NIC) katika Maonesho ya 46 Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akizungumza katika Banda la Shirika la Taifa la Bima (NIC) katika Maonesho ya 46 Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala akisaini kitabu katika Banda la Shirika la Taifa la Bima (NIC) katika Maonesho ya 46 Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
*Aitaka NIC ikutane na Watu wenye Masoko
Na Chalila Kibuda, Michuzi Blog
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amepongeza Shirika la Taifa la Bima(NIC) katika utoaji wa Bima kwa kutumia mifumo ya kisasa.
Makalla ameyasema hayo wakati alipotembelea Banda la NIC katika maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam (Sabasaba), Makala amesema kuwa katika kufanya kazi huko wawafikie wananchi wengi zaidi kupata huduma za bima.
Amesema kutokana na masoko kuungua NIC ikutane na watu wa masoko ili kuwapa elimu ya bima na kisha wafanyabiashara nao waweze kukata bima hizo.
Aidha amesema masoko yakiwa na bima pamoja na wafanyabiasha wakiwa na bima itafanya kuwa na biashara endelevu kwani inapotokea wanafidiwa bidhaa zao.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja Yesaya Mwakifulefule amesema kuwa wanaendelea na jitihada za kuwafikia wananchi pamoja na utoaji wa elimu.
Amesema kuwa katika utendaji wao wamekuwa na mifumo ya kisasa katika kutatua changamoto ya wateja pale pindi ambapo wanakuwa wamepatwa na majanga mbalimbali.
Aidha amesema Shirika limeweza kuanzisha bima zingine na kuachana mazoea ya bima ya magari ambapo sasa bima zinazopatikana ni pamoja na kilimo , Bima za Maisha pamoja Bima za Taasisi kwenye magari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...